Habari za Punde

Wafanyakazi wa Kada ya Utumishi na Rasilimali Watu Kupitia ICT Watakiwa Kuimarisha Miundombinu ya TEHAMA

Na.Kassim Abdi -WUMU.

Serikali zote mbili zimechukua jitihada za maksudi za kuweka miundombinu wezeshi katika matumizi ya teknolojia ya habari na mawasilaino ili kwenda sambamba na mabadiliko Duniani.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk. Khalid Salum Mohamed ameeleza hayo wakati akiufungua mkutano uliowshirikisha wafanyakazi wa kada ya Utumishi na rasilimali  watu kupitia ICT uliofanyika katika ukumbi wa Hotel Verde Mtoni Zanzibar.

Mhe. Waziri amesema Serikali zimetunga sera mahususi zenye kutoa kipaumbele kwa ajili ya uimarishaji wa miundombinu ya TEHAMA na matumizi yake ili kuweka mazingira bora ya kuikuza teknolojia ya habari na mawasilianpo mifumo ya mawasiliano sambamba na kuwawezesha wananchi wake kupata huduma bora na kwa haraka zinazotolewa na Serikali.

Aidha. Dk. Khalid amefafanua kwamba kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hivi sasa inaendelea  kuzifanyia mapitio sera zake zinazohusiana na masuala ya teknlojia ya habari na mawasiliano  ili ziendane sambamba na wakati uliopo.

Waziri Dk. Khalid amesema kuwa, Serikali kupitia wakala wa miundombinu ya TEHAMA tayari imeziunganisha tasisi pamoja na mashirika ya Serikali kwa takribani  Aslimia 98% hadi sasa ikizijumuisha uazishwaji wa vituo vya TEHAMA katika  na wilaya zote kumi na moja (11) za Zanzibar.

“Jambo zuri la kujivunia kwetu sisi Zanzibar tumepiga hatua kubwa ya kuziunganisha taasisi pamoja na kuanzisha vituo katika  wilaya zote kumi na moja Unguja na Pemba na Mkonga wa mawasiliano wa Taifa (Fiber Cable)” Alisema Mhe. Waziri

Pia, Mhe. Waziri amesema dira ya maendeleo ya taifa 2050 imeeleza kwa kuweka kipaumbele maalum cha kuimarisha sekta hiyo ya matumizi ya teknolojia ambapo baadhi ya huduma zimeanza kutolewa kwa kutumia mifumo ikiwemo huduma za Afya, Elimu, Malipo pamoja na huduma za matumizi ya mawasiliano ya simu.

Nae, Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Injinia Othaman Sharif Khatib amesema suala la mabadiliko ya matumizi ya teknolojia sio sula la kuchagua ila kila nchi inalazimika kuyapokea mbadiliko hayo kutokana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia ulimwenguni kote.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya madola ya mawasiliano Bernadette Lewis ameipongeza Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Jitihada inazozichukua katika kuwashajihisha watu wake juu ya mabadiliko ya matumizi ya teknolojia ya mawasiliano.

Amesema kuwa, Jumuiya ya madola imeamua kushirikiana na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  katika kutoa mafunzo kwa watu wake pamoja na wajumbe kutoka nchi wanachama lengo likiwa kuwajengea uwezo juu ya matumizi sahihi ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Jumla ya washiriki Mia moja na hamsini (150) kutoka nchi kumi na moja  wameshiriki katika Mkutano huo wa kuwajengea uwezo watendaji wa nchi wanachama.

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar.

17/05/2023.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.