Habari za Punde

Waziri Balozi Pindi Chana Azungumza na Viongozi wa Kimataifa Kuimarisha Ushirikiano Sekta ya Sanaa,Michezo na Uhifadhi wa Kihistoria

 

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe.  Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Kimataifa leo Mei 11, 2023 jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao ni pamoja na Naibu Balozi wa Uswisi hapa nchini, Bw. Leo Nascher, Naibu Balozi wa Hispania hapa nchini, Bw Jose Garcia na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO, Bw. Michel Toto.

Mazungumzo yao  yamelenga kuimarisha mashirikiano katika Sekta  ya Michezo, Sanaa katika  filamu pamoja na uhifadhi wa historia kupitia Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Dkt. Emmanuel Ishengoma, Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Dkt. Kiagho Kilonzo, Mratibu wa Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika, Bw. Boniface Kadili pamoja na Mwakilishi kutoka Idara ya Michezo, Bw. Benson Chacha.





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.