TANZIA:
Inna liyllahi wainna ilayhi rajiouna (Hakika Sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake Tutarejea).
Maalim Aboubakar bin Said (Maarufu Maalim Abuu) Ametangulia mbele ya Haki.
Maalim Abou ni Sheikhe Mkubwa katika visiwa vya Zanzibar.
Alikua ni Mwalimu wa Skuli akifundisha somo la Dini ya Kiislamu.
Ni maarufu sana kwa kuozesha katika Ndoa za Kiislamu huku akisoma Hutba ya ndoa kwa sauti ya Kuisisimua Hadhira.
Alikua ni Imam Mkuu katika Msikiti wa Mwembetanga unaojulikana kwa Masjid Shifaa awali ukiitwa Msikiti Maiti.
Kumujibu wa Familia ya Marehemu maziko yatafanyika kesho na kusaliwa Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini baada ya Sala ya Ijumaa.
Mwenyezi Mungu amsameh makosa yake,na ajaalie kaburi lake liwe ni miongoni mwa Bustani za Pepo.
No comments:
Post a Comment