Habari za Punde

KATIBU MKUU BW. SAIDI YAKUBU ASISITIZA WATENDAJI SEKTA YA SANAA KUWA UBUNIFU KATIKA UTENDAJI KAZI

 

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu (kulia) akipewa taarifa ya utendaji kazi na Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania na Mtendaji Mkuu Nyakaho Mahemba (kushoto) Juni 20, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi katika wa Mfuko huo.

Na Eleuteri Mangi, WUSM-Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amewasisitiza watendaji na watumishi wa taasisi chini ya wizara hiyo kuwahudumia wadau wa sekta ya Utamaduni na Sanaa kwa wakati ili kuleta tija katika utendaji kazi.

Katibu Mkuu Bw. Yakubu amesema hayo Juni 20, 2023 jijini Dar es Slaaam alipofanya ziara ya kikazi katika taasisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania pamoja na Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania.

"Tuongeze ubunifu zaidi na kurasimisha wafanyabiashara wa kazi za Utamaduni na Sanaa na wasanii ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika utoaji wa huduma kwa wadau wa sekta zetu hizi" amesema Bw. Yakubu.

Ameongeza kuwa taasisi zote za Wizara zina wajibu kutekeleza vipaumbele vya Serikali ikiwemo kuongeza wigo wa wasanii kwenda kufanya kazi za Sanaa nje ya nchi na kutangaza Utamaduni na Sanaa ya Tanzania na kuongeza ubunifu katika utendaji kazi wao.

Kwa upande wao Katibu Mtendaji wa BASATA Dkt. Kedmon Mapana, Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania Dkt. Kilonzo Kiagho pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania Nyakaho Mahemba wamesema taasisi zao zitatekeleza kwa vitendo maelekezo ya Serikali ili kuwahudumia wadau wao.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu (katikati) akipewa akitembelea ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wakati wa ziara ya kikazi katika katika taasisi hiyo.

Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania Dkt. Kilonzo Kiagho (katikati) akisisitiza jambo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu (wa kwanza kulia) alipofanya ziara ya kikazi katika taasisi hiyo Juni 20, 2023 jijini Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana akisisitiza jambo wakati wa kikao na wakati na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu alipofanya ziara ya kikazi katika taasisi hiyo Juni 20, 2023 jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.