Habari za Punde

KATIBU MKUU BW. YAKUBU AKUTANA NA MWAKILISHI WA SHIIRIKA LA ARIPO

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu (kulia) akiongea na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Miliki Bunifu la Kikanda Afrika (ARIPO) Bi. Flora Mpanju (katikati) Mei 31, 2023 katika Ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bi Doreen Sinare.

Na Eleuteri Mangi, WUSM Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amefanya kikao na Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Miliki Bunifu la Kikanda Afrika (ARIPO) Bi. Flora Mpanju Mei 31, 2023 katika Ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Bw. Yakubu amesema kuwa Tanzania inathamini na itaendelea kushirikiana na ARIPO katika sekta ya Miliki bunifu ambayo inamchango mkubwa katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Miliki bunifu Afrika (ARIPO) Bi Flora Mpanju amesema shirika hilo linathamini sana mchango wa Tanzania katika kazi zao kwa kuzingatia sifa nzuri na uaminifu katika shirika hilo iliyojengwa na Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere. 

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bi Doreen Sinare pamoja na watendaji wa taasisi hiyo ambapo amesisitiza kuwa COSOTA imeshatoa tangazo la Kampuni Ukusanyaji na Ugawaji Mirabaha ili kuboresha mazingira ya wasanii kunufaika na kazi zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.