SERIKALI ya Mapinduzi
ya Zanzibar imeahidi kuipatia Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) jengo jipya la
kisasa litakaloendana na hadhi ya tume hiyo sambamba na kupatiwa ofisi za tume kwa
ngazi zote za wilaya na Ofisi kuu ya Pemba kwenye bajeti ya mwaka mpya wa fedha,
2013/2024.
Pia, Serikali
imeahidi kuzifanyia kazi changamoto zinazoikabili tume hiyo ikiwemo kuboresha
maslahi ya watendaji wake hasa kwenye suala zima la marekebisho ya mishahara
ambapo imeeleza tayari imetoa maagizo na kuahidi utekelezaji wake.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi alitoa ahadi hizo
alipozungumza na Tume hiyo, Ikulu Zanzibar iliyofika kwa lengo la kumuarifu rasmi
Rais kumaliza kazi, kufuatia kukamilika miaka mitano ya utumishi wake.
Dk. Mwinyi aliipongeza
tume hiyo kwa ushirikiano walioutoa kwa wadau mbalimbali wakiwemo vyama vya
siasa nchini pamoja na kufanikiwa kutangaza matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020 ndani
ya saa 24 baada ya uchaguzi kumalizika.
Vile vile, Rais Dk.
Mwinyi alisema Serikali inajipanga na kuifanyia kazi changamoto ya vyombo vya
usafiri inayoikabili tume hiyo na kuahidi kuongeza bajeti itakayofanikisha
utendaji wa tume hiyo.
Akizungumza kwenye
hafla hiyo, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Hamid Mahmoud, alisema tume
ilipewa majukumu ya utendaji wake chini ya sheria tatu ambazo ni Sheria ya
kuanzisha ofisi ya Tume ya Uchaguzi sheria nambari moja ya mwaka 2019, Sheria
ya uchaguzi nambari nne ya mwaka 2018 pamoja na Sheria ya kura ya Maoni nambari
sita ya mwaka 2000.
Alisema, Sheria
inaitaka tume hiyo kumkabidhi ripoti ya utendaji Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi mara baada ya kukamilisha muda wake wa utumishi.
“Kwamujibu wa kifungu
namba 27 cha 3 cha sheria nambari moja ya mwaka 2017, sheria ya kuanzisha tume
halisi ya uchaguzi, kinaitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, kuwasilisha ripoti
ya miaka mitano kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mara
baada ya kumaliza kazi iliyopewa kwa kipindi husika”. Alifafanua Mwenyekiti
huyo.
Mbali na mafanikio
makubwa iliyofikiwa, tume hiyo ilimueleza Rais Dk. Mwinyi kwamba ilifanikiwa kuanddaa
muundo mpya wa ofisi ya tume uliotoka kwenye utumishi wa tume hiyo, ukiwemo muundo
wa mishahara uliozingatia maslahi ya watumishi wa tume.
Pia tume hiyo,
ilimueleza Dk. Mwinyi kwamba ndani ya miaka mitano ya utumishi wake ilifanikiwa
kufanyakazi kwa ushirikiano na ufanisi mkubwa na vyama mbalimbali vya Siasia
nchini pamoja na kufanikiwa kuandaa mpango mkakati wa miaka mitano kuanzia
mwaka 2022 hadi 2026.
Aidha, tume hiyo
ilieleza kufanikiwa kuandaa na kusimamia uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, kupitia fedha
za mfuko mkuu wa serikali na ilifanikiwa kutekeleza haki na misingi ya
demokrasia kwa kushirikisha matumizi ya tehama na ushirikishwaji wa wadau
katika masuala yote ya uchaguz na kwa mara ya kwanza walitoa matokeo ya
uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ndani ya masaa 24 tokea uchaguzi kukamalizika jambo
walilolielza kwamba halikuwahi kufanyika awali.
Licha ya mafanikio
hayo, pia tume hiyo ilimueleza Rais Dk. Mwinyi changamoto iliyokumbana nazo ndani
ya kipindi cha miaka mitano ya utendaji wake.
Ilisema, kazi ya
uhakikishaji wapiga kura ilikwenda sambamba na kazi ya ugawaji wa vitambulisho
vya Mzanzibari mkaazi (ZAN ID) kwa baadhi ya maeneo, hali waliyoieleza kwamba iliathiri
sana zoezi la uandikishwaji wa wapiga kura.
Tume hiyo pia
ilieleza kwamba inakabiliwa na changamoto kubwa ya kutokua na ofisi za uhakika
kwa Unguja na Pemba hata kwa ndazi za Wilaya, hali waliyoeleza kwamba baadhi ya
shughuli za tume hiyo kuathiri utendaji ikiwemo chamgamoto ya vyombo vya
usafiri na maslahi ya watendaji wake pamoja na ukosefu wa bajeti ya ujumla hasa
kwa asasi za kiraia.
Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar (ZEC) inayomaliza muda wake, awali ilichaguliwa Juni 20, mwaka 2018
ikiwa na Mwenyekiti wake na wajumbe sit ana sasa imebakiwa na Mwenyekiti wake
na wajumbe watano kufuatia Mjumbe mmoja bw. Makame Juma kufariki mwaka Novemba 21 mwaka 2021.
No comments:
Post a Comment