Habari za Punde

Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria yatakiwa kuwa makini

Naibu Mwana Sheria Mkuu  Zanzibar Shaaban Ramadhan Abdalla  akizungumza na wadau wa sheria wakati akifungua mhadhara unaohusu misaada ya kisheria ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za kuelekea kilele cha wiki ya msaada wa kisheria ambayo inatarajiwa kufanyika Julia 22,mwaka huu,Hafla iliyofanyika  Ofisi ya Katiba na sheria Mazizini Zanzibar Julia,18,2023. PICHA NA FAUZIA MUSSA- MAELEZO ZANZIBAR
Mkuu wa Skuli ya Sheria Zanzibar  Dkt.Ali Ahmed Uki akiwasilisha mada ya masuala ya msaada wa kisheria wakati wa mhadhara wa wadau wa sheria uliofanyika  Ofisi ya Katiba na Sheria Julia 18 ikiwa ni shamrashamra kuelekea kilele cha wiki ya msaada wa kisheria  inayotarajiwa kufanyika Julia 22 mwaka huu.PICHA NA FAUZIA MUSSA- MAELEZO ZANZIBAR
Mkurugenzi jumuiya ya wasaidizi wa sheria Wilaya ya Mjini Yunus Juma Ali Akichangia mada ya masuala ya msaada wa kisheria wakati wa mhadhara  uliofanyika Ofisi za Katiba na Sheria julai 17,2023 ikiwa ni shamrashamra kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria inayotarajiwa Kufanyika Julia 22 mwaka huu.PICHA NA FAUZIA MUSSA- MAELEZO ZANZIBAR
Msaidizi wa Sheria Fatma Khamis Ali Akichangia mada ya masuala ya msaada wa kisheria wakati wa mhadhara  uliofanyika Ofisi za Katiba na Sheria julai 17,2023 ikiwa ni shamrashamra kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria inayotarajiwa Kufanyika Julia 22 mwaka huu.PICHA NA FAUZIA MUSSA- MAELEZO ZANZIBAR

 Na Rahma Khamis Maelezo   

Naibu Mwanasheria Mkuu Zanzibar Shaaban Ramadhan Abdalla  ameitaka Idara ya Katiba na  Msaada wa Kisheria kuwa makini katika kutekeleza majukumu yao ili kufikia malengo waliojiwekea.

Ameyasema hayo katika Ukumbi wa Katiba na Sheria Mazizini wakati akifungua  mhadhara wa Msaada wa kishria ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa kisheria.

Amesema kufanyika kwa mhadhara huo kutasaidia wahusika wa sheria  kupata elimu zaidi na kuweza kutekeleza majuku yao kwa ufanisi mkubwa.

Aidha amefahamisha kuwa ni vyema kwa washiriki katumia fursa hiyo kwa kuskiliza kwa umakini  ili kupata elimu  zaidi na kufahamu jinsi ya kuendeleza kazi zao ili kufikia malengo

"Ni  vizuri tukatumia  fursa hii ,tuwe makini kusikiliza ili tupate  yale mazuri ambayo yanetegemewa na kupata uzoefu zaidi tuendeleze tuliyojifunza  tuweze kuyafanya kazi  sehemu yeyote Unguja na Pemba ,"alisistiza Naibu.

Katika hatua nyengine  Naibu amemshauri Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa Sheria kuendeleza jitihada hizo na kuwaendeleza wafanyakazi  kimafunzo ili kusaidia jamii  kupata haki zao.

Nae Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Hanifa Ramadhan Said  amesema kuwa madhumuni ya mhadhara huo ni kujifunza na kupeana uzoefu wa utoaji wa mswaada wa kisheria  kwa vile  wamo katika kuadhimisha wiki ya Maswada wa kisheria ili kuweza kufahamu matatizo yanayowakabili  na kuyapatia ufumbuzi.

Akitoa mada ya Mswaada wa Kisheria katika mhadhara huo Mkurugenzi Skuli ya Sheria Dkt Ali Ahmed Uki amesema wasaidizi wa sheria wanatoa mswaada mkubwa na wameiasaidia jamii kupata haki kwa wasio na uwezo bila ya kuzingatia rangi na kabila zao.

"Wasaidizi wa sheria wanastahiki sheria kupongezwa kwa kujitolea kutoa huduma za sheria bila a malipo licha ya chanagamoto wanazokumbana nazo kawni jamii imewakubali sana"alifahamisha Dkt auaki.

Aidha amesema kuwa matatizo mengi  yanayojitokeza katika jamii ni matatizo ya ardhi jambo ambalo limepelekea kuwekwa kwa Mahakama na wasaidizi wa sheria ya Ardhi ili kupunguza tatizo hilo kwani Mahakama hiyo inasaidia kwa kiasi kikubwa.

Nao washiriki wa mhadhara huo wameiomba Serikali kuweka mikakati maalum ya kuhakikisha usalama kwa  wasaidizi wa Kisheria kwani wanakumbana na matatizo mengi katika  kazi zao  wanazozifanya ikiwemo vitisho ,viashiria vya udhalilishsaji ,kuitwa majina mabaya na kutukanwa jambo ambalo linarejesha nyuma jitihada za kuwasaidia watu kuweza kupata haki zao.

Wamesema kuwa kwa kiasi fulani wameweza kupiga hatua kwani wamekuwa wakishirikiana na wadau tofauti ikiwemo Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) Zanzibar na Chama cha Wanasheria Wanawake ( ZAFELA) katika kufanya kazi zao na kufikia malengo.

Hata hivo wameiomba Serikali kuwasimamaia watoto waliopata matatizo ya udhalilishaji  kuwewekea kitengo maalumu ili kuwasaidia  na  kuwaondoshea vikwanzo vikwwanzo dhidi yao na kujiona kuwa wako sawa na wenzao.

Mhadhara huo wa siku moja umeandaliwa na Idara ya katiba na msaada wa sheria ukiwashirikisha wasaidizi wa Sheria kutoka Mjini na Vijijini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.