Habari za Punde

Madaktari Bingwa kutoka nchini Ujerumani kuwasili Tanga Julai 13 mwaka huu

Na Oscar Assenga,TANGA                                                                                                                          

MADAKTARI Bingwa kutoka Nchini Ujerumani wanatarajiwa kuwasili Mkoani Tanga kesho Julai 13 ambao wanakuja kwa ajili ya kutoa huduma za Kibingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga –Bombo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Tanga leo,Mratibu wa Kambi ya Upasuaji wa Kurekebisha Maumbile (Plastic Surgery) kwenye Hospitali hiyo Dkt Wallace Karata alisema madaktari hao watakuwepo hadi Julai 28 mwaka huu na siku inayofuatia wataondoka nchini.

Dkt Karata alisema kwamba madaktari hao wanakuja kutoa huduma kwa watanzania ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu lakini pia kwa fani yao ya upasuaji na kurekebisha maumbile ambayo haipatikani vya kutosha nchini na hivyo wanakuja kutoa bure kama msaada kwa watanzania.

Alisema hadi sasa wagonjwa 200 wamekwisha kujiandikisha na wakiwa tayari kwa ajili ya kusubiri huduma na Julai 10 ilikuwa ni mwisho kujiandikisha na wageni hao watakapoingia Julai 14 watafanya uchunguzi wa awali na kuweza kupanga ratiba za upasuaji.

Dkt Karata alisema operesheni zitaanza Julai 17 hadi Julai 28 kabla ya wageni hawajaondoka nchini hivyo waliojiandikisha wasishaua tarehe waliozopewa ili kuepukana na usumbufu wa kupanga ratiba zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.