Habari za Punde

Multichoice Yawanoa Watunzi wa Filamu Zanzibar

 

Multichoice Talent Factory Kwa kushirikiana na ZIFF wameandaa mafunzo kwa wasanii wa maigizo Kwa lengo la kuinuka na kuikuza sanaa ya filamu.

Mafunzo hayo yamefanyika katika hoteli ya Serena mjini Unguja ambapo takriban watunzi 37 wa filamu kutoka Tanzania bara na Zanzibar wamepatiwa elimu hiyo.

Akizungunza na waandishi wa habari Mkurungenzi wa Multichoice Africa Bi. Nwabisa Matyunza amesema Sanaa Kwa upande wa Zanzibar bado ipo chini sana kutokana na ukosefu wa elimu ya kitaalumu hasa Kwa watunzi jambo linalopelekea kushuka Kwa Sanaa visiwani humo.

Aidha ameongeza kuwa matarajio yao baada ya mafunzo hayo wasanii watafanya kazi zenye ubora na kufika viwango vya kimataifa.

Kwa upenda wake Mkurungenzi wa ZIFF Ndugu Martin Muhando ameishukuru Multichoice kwa ushirikiano wao wa kukuza vipaji vya wasanii na kuhakikisha wanafika viwango vya juu.

Nae Katibu wa Bodi ya filamu Tanzania Kiagho Kilonzo amesema Serikali itaendelea kushirikiana na watasisi mbalimbali zenye kuboresha sanaa ambayo itatoa ajira nzuri Kwa vijana na kuleta tija Kwa taifa.

Mshiriki wa mafunzo hayo ndugu Damas Donad amesema wataitumia vyema elimu hio Kwa kuandika story zenye viwango, ubora na maadili Ili kuendana na soko la Sasa la Dunia.

Mafunzo hayo ya siku mbili yameandaliwa na Africa Multichoice Talent Factory Kwa kushirikiana na ZIFF pamoja na bodi ya filamu Tanzania ambapo Kwa Tanzania ni mara ya pili kufanya mafunzo kama hayo. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.