Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya Pasific, Mhe. Harjit Sajjan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo
Waziri wa
Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya
Pasific, Mhe. Harjit Sajjan akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo baada ya
kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es
Salaam
Waziri wa
Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya
Pasific, Mhe. Harjit Sajjan akimsikiliza
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam
Waziri wa
Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya
Pasific, Mhe. Harjit Sajjan akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya Pasific, Mhe. Harjit Sajjan amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano kuanzia tarehe 19 – 23 Julai, 2023.
Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Mhe. Sajjan alipokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo.
Akiwa nchini, Mhe. Sajjan pamoja na ujumbe wake anatarajia kukutana na viongozi mbalimbali wa Serikali na kujadiliana nao masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na Canada.
Aidha, Waziri Sajjan anatarajia kukutana kwa
mazungumzo na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Waziri wa Afya pamoja na
kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Canada.
No comments:
Post a Comment