Habari za Punde

Flight Link kuanza safari za Arusha - Zanzibar

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Simai Mohammed Said akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe Omar Said Shaaban wakiwa pamoja na uongozi wa Flight Link katika hafla ya chakula cha usiku iliofanyika hoteli ya Grand Melia Arusha, Tanzania.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Simai Mohammed Said akizungumzia wakati wa uzinduzi wa ndege mpya kampuni ya Flight Link, katika hafla ya chakula cha usiku iliofanyika hoteli ya Grand Melia Arusha, Tanzania.
Ndege ya Flight Link ambayo itaanza safari za moja kwa moja Arusha - Zanzibar 

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Simai Mohammed Said ameshiriki katika uzinduzi wa ndege mpya kampuni ya Flight Link, katika hafla ya chakula cha usiku ilofanyika hoteli ya Grand Melia iliyopo Arusha, Tanzania.

Kampuni hiyo ya Flight Link ilianzishwa mwaka 2001 na ilianza safari zake ndani ya Tanzania katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Dodoma hadi mwaka 2016 ilipotajwa kuchukua nafasi ya 5 katika usafiri wa anga Tanzania.
Mwaka 2022 kampuni hiyo iliongeza uwezo wake kiutendaji na kuanzisha safari za Mombasa - Kenya na kwa sasa imeanzisha safari za moja kwa moja kutoka Arusha - Zanzibar kwa lengo la kuwatoa wageni kutoka Serengeti - Arusha - Zanzibar ambapo soko kubwa la utalii litafunguka na wageni watapata huduma stahiki ya moja kwa moja.
Meneja wa kampuni hiyo amesema kampuni hiyo imeboresha zaidi kwenye miundo yao ambapo kwa sasa wana idara ya Teknolojia ya habari (Information Technology Department), idara ya rasilimali watu (Human Resource department) na idara ya huduma za dharura (emargency department) katika kuhakikisha umakini wa kiutendaji na watendaji wao, wakiwa na kauli mbiu ya " Ndege zenye upekee na huduma bora (Airline with distinction and exellency).
Nae Mhe. Simai aliwapongeza sana kwa jitihada zao na aliwataka waendelee kukuza ushirikiano katika sekta ya utalii na ikiwezekana waanzishe helikopta kwa ajili ya wageni maarufu (VIP Tourists) ili kutoa huduma bora.
Mhe. Simai ametoa wito kuwa Tanzania ina maeneo mengi sana ya utalii ambayo hakuna huduma za kuaminika za ndege hivyo wana fursa kubwa ya kufikiria maeneo kama ziwa Tanganyika, njombe, tarangire na pia Pemba ambapo amesema baada ya Kumalizika uwanja wa ndege wa Pemba, kutakua na fursa nyingi hivyo Fight link na kampuni nyengine za uwekezaji hasa katika sekta hii ya utalii, ni vyema wakatumia fursa hiyo

"Ni wakati wa kubadilisha mtazamo wetu kwa pande zote mbili Tanzania bara na Visiwani, na kuhakikisha ushirikiano wa mabadiliko haya unaleta tija katika kukuza utalii wetu. Watalii watapenda pia kuogelea huku wakinyeshewa na mvua kama moja ya kivutio kikubwa kwao (adventure) ambapo kutawafanya wafurahie uwepo wao hapa nchini" .amesema Mhe Waziri

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.