RAIS
wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewaasa Watanzania
waliokabidhiwa vyeti kwa Tajnisi kuendeleza utiifu wa sheria na kuendelea kusihi kwa
kujiepusha na vitendo viovu ili wasipotoshe dhamira njema ya Serikali ya kupewa
uraia wa Tanzania.
Dk. Mwinyi alitoa nasaha hizo Ikulu, Zanzibar alipowakabidhi vyeti kwa tajinisi Watanzania 3319, wahamiaji wasiohamishika baada ya kukidhi vigezo na Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa raia halali nchini.
Rais Dk.
Mwinyi aliwataka Watanzania hao kuipa heshima inayostahili hadhi waliyopewana
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwa raia, kwa kuwa raia wema.
“Kwa
hakika ndugu zangu mna wajibu kwa pamoja tushirikiane kulinda na kudumisha
amani tuliyonayo kwa faida yetu, tuliopo sasa na wale watakaokuja baadae”
aliwaasa Watanzania hao
Rais Dk. Mwinyi aliwahakikishia
Watanzania hao kuwa na haki zote baada ya kuthibitishwa uraia wao kama
wanazostahili raia wengine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia,
aliwaasa kuzitumia vyema haki na fursa hizo kwa kushiriki kikamilifu kwenye
harakati za maendeleo kwa ustawi wa familia zao na Taifa kwa jumla na kuwataka
ambao hawajajisajili kufanya hivyo kwa mamlaka husika.
“Natumia nafasi hii kutoa wito kwa ndugu zetu
ambao kwa namna moja au nyengine hawajafika kwenye Ofisi za Uhamiaji
kujiorodhesha, ni vyema wakaitumia fursa hiyo ili watambuliwe rasmi, Serikali
zetu zimedhamiria kulimaliza tatizo hili kutokana na athari zake”. Aliwasihi
Dk. Mwinyi
Sambamba
na kuzitaka mamlaka za Serikali na Binafsi kuwapa ushirikiano Watanzania hao
kwenye masuala mbalimbali kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na iongozo iliyopo kama
wanavyofanyia Watanzania wengine.
Katika hatua nyengine Rais Dk. Mwinyi alitoa wito
kwa Idara ya Uhamiaji, kuendelea kuziimarisha sheria zilizopo hususan
Sheria ya uraia wa Tanzania kwa kuifanyia mapitio kwa madhumuni ya kuiwezesha
kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowahusu wananchi na wageni wanaofika
nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni
Yussuf akizungumza kwenye hafla hiyo alizipongeza Serikali za Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania nay a Mapinduzi ya Zanzibar kwa busara zao za kuwasahe
Watanzania hao kiasi cha milioni mbili kama kima cha kulipia uraia wao pamoja
na kupongeza ushirikiano kwa Serikali mbili hizo kulifanikisha jambo hilo.
Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Hamza Hassan Juma alimpongeza
Rais Dk. Mwinyi kwa kukamilisha ahadi ya kuzitatua changamoto za Wanzania hao
wahamiaji wasiohamishika tangu alipowaahidi mwaka 2020 kuitekeleza kwa vitendo
ahadi yake ya kushughulikia changamoto za Watanzania hao.
Kwa upande wake, Kamisha Jeneral wa Uhamiaji
Tanzania, Dk. Anna Makakala alisema jeshi hilo linajukumu la kuratibu masuala
yote ya uhamiaji nchini yanayohusu raia wanaoomba uraia kisha kukabidhi kwa
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi.
Aidha alieleza Idara ya Uhamiaji Zanzibar kwa
kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilifanya zoezi la utambuzi
kwa Watanzania hao mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Watanzania hao waliokuwa wakikabiliwa na
changamoto za kukosa haki zao za msingi kisheria zikiwemop hati za uraia, hati
za kusafirikia na haki nyengine wanazopatiwa Watanzani halisi.
Jumla ya Watanzania 3319 wenye asili ya mataifa
mbalimbali waliokua wahamiaji wasiohamishika wametambuliwa rasmi na Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kuwa raia halali wa Tanzania. Miongoni mwao 3116 wanaasili
ya Msumbiji, 147 wanaasili ya visiwa vya Komorao, watano kutoka Burundi na raia
mmoja kutoka Jamhuri ya Rwanda, aidha watoto 1675 pia walitambukliwa
IDARA YA MAWASILIANO
IKULU, ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment