Habari za Punde

Jamii Yashauriwa Kufuata Maelekezo ya Wataalamu wa Afya Ili Kujikinga na Maradhi Yasioambikiza

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Hassan  Khamis Hafidh Akizungumza na Waandishi wa Habari katika kilele cha  maadhimisho ya wiki ya maradhi yasioambukiza  ambayo huanzia septemba  14 hadi  21  Kila mwaka Duniani kote, hafla iliyofanyika  Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Unguja .
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Fatma Mrisho akimshauri Jambo Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh katika kilele cha  maadhimisho ya wiki ya maradhi yasioambukiza ambayo huanzia septemba  14 hadi  21  Kila mwaka Duniani kote , hafla iliyofanyika  Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Unguja .

Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Mnazimmoja Dkt.Amour Sleiman Mohammed akichangia katika kilele cha  maadhimisho ya wiki ya maradhi yasioambukiza ambayo huanzia septemba  14 hadi  21 Kila mwaka Duniani kote, hafla iliyofanyika  Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Unguja .

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR 

Na Fauzia Mussa,    Maelezo

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh amewataka Wananchi kufuata   ushauri  unaotolewa na wataalamu wa Afya kuhusu kujilinda na magonjwa yasioambukiza ili kushinda vita dhidi ya magomjwa hayo.

 

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika kilele cha wiki ya magonjwa  yasioambukiza Naibu Hassan alisema  kufanya hivyo kutapunguza wimbi la wagonjwa wa maradhi hayo wanaoongezeka siku  hadi siku duniani kote  .

 

Alisema  kwa upande wa Zanzibar magonjwa hayo yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku na kusababisha vifo ,ulemavu pamoja na kuongeza utegemezi wa wagonjwa kwa familia kutokana na kuuguwa kwa muda mrefu.

 

“Wahenga walisema kinga ni bora kuliko tiba ,tuna kila sababu ya kujikinga na maradhi  yasioambukiza hasa ukizingatia maradhi haya yanaweza kukingwa kwa kufuata ushauri wa wataalamu wa afya” Alisistiza Naibu huyo

 

Alisema katika kuadhimisha wiki hiyo Wizara kupitia kitengo cha maradhi yasioambukiza kwa kushirikiana na Taasisi ya Pham Acces iliendesha zoezi la upimaji wa Afya kwa Wananchi wa  Unguja na Pemba ambapo  Takwimu zilithibitisha hali halisi ya Magonjwa hayo visiwani.

 

 Alifahamisha kuwa  kati ya watu 747 waliochunguzwa, watu 19 sawa 2.5% waligundulika kuwa na kiwango kikubwa cha sukari, Watu 84 sawa na 11.2% waligundulika kuwa  na shindikizo la juu la damu (Presha) na watu 124 sawa na 16.6% walionekana kuwa na uzito uliopindukia,

 

hivyo alisema ipo haja ya kushirikiana na  kuongeza juhudi katika kupambana na Magonjwa hayo ili kuyatokomeza nchini

 

Sambamba na hayo  aliwataka wananchi kubadilisha mfumo wa chakula kwa kujitahidi kula mlo kamili unaofaa, kufanya mazowezi, pamoja na kuachana na vichocheo vyote vya maradhi yasioambukiza ili kuwa na Taifa lenye wananchi wenye Afya bora.

 

“tunajua kuwa katika  jamii kubwa kama hatujala chipsi haturidhiki,tena inaliwa usiku halafu tunalala, tujue tunashibisha tumbo lakini tunakaribisha maradhi mengi ikiwemo

yasioambukiza”alikumbusha Naibu huyo.

 

Nae Mwakilishi wa  Taasisi ya PharmAcces Queen – Ruth Msina ameishukuru Serikali kwa kuthamini na kujali mchango wao wanaoutoa katika kupambana na vita dhidi ya magonjwa yasiambukiza

 

Wiki ya Magonjwa  yasioambukiza  huanza Kila ifikapo septemba 14 na kufikia kilele chake septemba 21 Duniani kote ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni  “ Muda wa Kujali Kuhusu Maradhi Yasioambukiza”.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.