Habari za Punde

Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Mjini Magharibi Kuanza Septemba 23, 2023

Na.Mwandishi Wetu.

LIGI Daraja la Pili Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, inatarajia kuanza Septemba 23, mwaka huu,kwa kuchezwa michezo mitatu katika viwanja vitatu tofauti.

Ligi hiyo ambayo inashirikisha timu 25 zilizopangwa katika makundi mawili inatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo inaonesha kuwa kwa siku kutakuwa na michezo mitatu ambayo itachezwa katika viwanja vya Mao Zedong, Nyamanzi na Maungani.

Katika uwanja wa Mao Zedong ratiba hiyo inaonesha kuwa katika uwanja wa Mao Zedong A kutakuwa na mchezo kati ya Danger na Eleven Star, mchezo ambao utachezwa majira ya saa 7:00 za mchana.

Aidha katika uwanja wa Kiembesamaki Jang'ombe Boys itakuwa uso kwa uso na timu ya Kijangwani, wakati katika uwanja wa Ngome Lion kids itapambana na Mbweni Academy.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.