Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kuhusiana na Mkutano wa Vijana wa Kimataifa wa Utalii Zanzibar, unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao Jijini Zanzibar, mkutano huo na waandishi uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Serena Zanzibar Shangani Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.
NA MADINA ISSA
SERIKALI ya mapinduzi ya zanzibar imesema itahakikisha watendaji wakuu wa serikali wadau mbalimbali wa maendeleo vijana na jamii kwa ujumla wanashiriki kivitendo katika mkutano wa vijana wa kimataifa wenye lengo la kuwainua vijana kupitia sekta ya utalii .
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Mohamed Said, aliyasema hayo alipokuwa akitoa taarifa ya mkutano wa vijana wa kimataifa wa utalii zanzibar unaotarajiwa kuanza tarehe 6 hadi 10 mwezi October huko katika ukumbi wa Serena Mjini Unguja.
Alisema serikali kupitia wizara ya utalii unaunga mkono juhudi zinazochukuliwa na vijana ambao inaisaidia serikali kuitanga zanzibar kwa kuifungua kiutalii kimataifa.
Aidha aliwasisitiza vijana kuwa wazalendo na kuendelea kuchangamkia fursa ambazo zitawawezesha vijana kujiimarisha kupitia sekta utalii ikiwemo ajira.
Sambamba na hayo, wliwahimiza vijana hao kuwa mabalozi mazuri kwa vijana wenzao ili kuweza kushiriki kikamilifu katika mkutano huo.
Mapema Muanzilishi Mwenza na Mkuu wa Mawasiliano wa Zanzibar international youth tourism sammirty, Abdulhamid Mzee, alisema lengo la kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kutoa uelewa kwa vijana kupitia sera ya uchumi wa buluu kuwainua vijana na wanawake wajasiriamali kupitia utalii kwa kufanya makongamano mbalimbali ambayo yataonesha njia na fursa za kuimarisha utalii kupitia vijana
Mkurugenzi wa taasisi ya zanzibar international youth tourism summity Mafunda Kombo Faki, alisema kupitia utalii mkutano huo utaonesha nafasi kwa vijana katika utalii endelevu ambapo mpaka sasa kuna idadi kubwa ya vijana ambao wameweza kujitokeza ili kushiriki mkutano huo.
Wakati huo huo Mhe.Waziri Simai, alimtambulisha na kumpongeza balozi wa vijana katika bodi ya utalii Afrika Mafunda Kombo Faki.
Hivyo, alimtaka kufanya kazi za kibalozi ili kuendelea kuitangaza Tanzania na vivutio vilivyopo nchini kupitia ubalozi wake.
Mkutano huo wa kimataifa utazihusisha nchi 13 zinarajiwa kushiriki ambapo zaidi ya vijana 150 watashiriki mkutano huo.
No comments:
Post a Comment