Watendaji na Viongozi wa umoja wa Wanawake Zanzibar wametakiwa kuwafuatilia wanaobeba wagombea (makundi ) na kuwafikisha katika Kamati za maadili ili waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria.
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania ( UWT ) Ofisi ya Zanzibar Tunu Juma Kondo Wakati alipokuwa akifungua mafunzo elekezi kwa Watendaji na Viongozi wa UWT Mkoa wa Magharibi kichama huko katika ukumbi wa CCM Kiembesamaki.
Amesema Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wameshachaguliwa katika uchaguzi uliopita hivyo wanatakiwa kushirikiana nao ili waweze kuwaletea maendeleo .
Amefahamisha kuwa UWT haitomvumilia mtu yoyote atakaebainika kubeba wagombea na hawatosita kumuondosha katika nafasi yake.
Aidha amewataka kuyafanyia kazi kwa vitendo mafunzo waliopewa ili yaweze kuleta tija katika chama na Taifa kwa ujumla.
Mbali na hayo amewataka kuwasilisha matatizo ya wanawake wenzao katika vikao Hali ili kuondosha majungu , fitna na uhasama miongoni mwao.
Vilevile amewahimiza kulipa ada kwa Wakati , kushiriki katika vikao na kuandaa Mikakati ya kupita nyumba kwa nyumba kuhamasisha Wanawake kujiunga na UWT ili kuweza kupata Wanachama wengi zaidi.
Sambamba na hayo amewataka Watendaji na Viongozi hao kuandaa miradi mbali mbali ya maendeleo, waweze kupata kipato kitakachoweza kuendesha katika harakati za maendeleo katika chama.
Akiwasilisha mada ya udhalilishaji wa kijinsia Mkurugenzi wa Idara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto Siti Abasi Ali amewataka wazazi na walezi kuwa makini katika malezi ya watoto na kuacha kutoa talaka kiholela ili kuondosha vitendo vya udhalilishaji kwa watoto wao.
Hata hivyo amewataka Wanaume kutowaachia mzigo mkubwa wa malezi wanawake ili kuwalinda na kuwakinga na vitendo vya udhalilishaji watoto wao.
Mbali na hayo amewaomba kuwaachia wake zao kufanya biashara ili waweze kusaidiana na kupata kipato Cha kuendesha maisha yao.
Mapema akimkaribisha Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Magharibi kichama Fatma Ali Ameir amesema lengo la kuandaa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Watendaji na Viongozi ili waweze kubadilika na kufanya kazi kwa ufanisi na kuepukana na kufanya kazi kwa mazoea.
Mbali na hayo amewaomba kusikiliza kwa makini mafunzo waliopewa na kuweza kuyafanyia kazi kwa kuwa mabalizi wazuri kwa wenzao na kuungana pamoja katika kuimarisha Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake.
Amewapongeza Wawakilishi na Wabunge wa Mkoa wa Magharibi kwa kuweza kutoa michango yao ya Hali na Mali na kufanikisha kufanyika kwa mafunzo hayo yatakayowawezesha Watendaji na Viongozi kufanya kazi kwa Ari na bidii ya Hali ya juu.
Mafunzo hayo elekezi kwa Watendaji na Viongozi wa UWT Mkoa wa Magharibi kichama ambapo jumla ya mada 3 ziliwasilishwa ikiwemo Oganizasheni ya vikao vya chama na Jumuiya, Udhalilishaji wa kijinsia na Uanzishaji wa miradi ya kimaendeleo
No comments:
Post a Comment