Habari za Punde

Mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar "PBZ Premier League 2023/2024" Kati ya Zimamoto na New City Uwanja wa Mao Zedung Timu Hizo zimetoka Sare ya Bao 1-1Beki wa Timu ya Zimamoto Amour Haji akiondoa mpira eneo la golini kwao huku mshambuliaji wa Timu ya New City na Joseph Mbaga akijaribu kumzuiya wakati wa  mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar "PBZ Premier League  2-23/2024, mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.Timu  hizo zimetoka sare ya bao 1-1. 

MAAFANDE wa timu ya soka ya Zimamoto wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na timu ya New City katka mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar uliochezwa juzi uwanja wa Mao Zedong A.

Mchezo huo ulioanza kwa kila mmoja kuusoma mchezo wa mwenziwe ulichezwa majira ya saa 10 za jioni na kuhudhuriwa na mashabiki kiasi.

Katika mchezo huo miamba hiyo pamoja na kucheza kwa kusomana lakini kila ambae alikuwepo uwanjani hapo aliridhika na viwango vya wachezaji walivyokuwa wakivionesha.

Timu hizo ambazo zililengeana mashambulizi zilikwenda mapumziko wakiwa hakuna ambae aliliona lango la mwenziwe.

Katika mchezo huo Zimamoto ndio waliotangulia kupata bao dakika ya 50, bao ambalo lilifungwa na mchezaji wao Ibrahim Hamad Hilika.
Kuingia kwa bao hilo kulizidisha mashambulizi kwa upande wa New City na kufanikiwa kusawazisha mnamo dakika ya 62.
Bao hilo ambalo lilionekana kuwachanganya Zimamoto liliwekwa kimiyani na mchezaji wake Nyai Shida Yohana.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo kwa kuchezwa michezo mitatu ambayo miwili itakuwa katika uwanja wa Mao Zedong A na B na moja itachezwa uwanja wa Finya.
KOCHA Msaidizi wa timu ya soka ya Zimamoto Mohammed Salahi 'Richcard' amesema kuwa baada ya kumaliza mchezo na New City wanarudi kujipanga ili kuhakikisha mchezo kati na Mafunzo wanapata matokeo mazuri.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mchezo huo ulimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1, alisema bado timu yao sio mbaya na ni matumaini yao kuwa mchezo huo na Mafunzo utawapa matokeo.

Hivyo alisema kuwa anaamini wakishirikiana wenyewe watafanya vizuri zaidi katika mchezo huo.

Hivyo aliwataka mashabiki kuona kwamba hii ligi bado ni mbichi na timu yao ipo katika hali nzuri ya kiushindani.

Timu ya Zimamoto inatarajia kushuka dimbani Septemba 24 mwaka huu, kucheza na Mafunzo.

Katika mchezo wake wa kwanza timu hiyo ya Zimamoto ambayo juzi ni mchezo wake wa pili, iliifunga Ngome mabao 5-0.
Mchezaji wa Timu ya Zimamoto Amour Juma (kushoto) na Mchezaji wa Timu ya New City Abdulhamid Ramadhan, wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar "PBZ Premier League 2023/2024" mchezo uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung Wilaya ya Mjini Ungyuja Jijini Zanzibar.Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
Kipa wa Timu ya New City Deogratus Mbabedi akiokoa moja ya michumo golini kwake, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Znzibar "PBZ Premier League 2023/2024, mchezo uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung.Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1. dhidi ya Zimamoto. 

Wachezaji wa Timu ya New City wakitafakari baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza mchezo wa Ligu Kuu ya Zanzibar "PBZ Premier League 2023/2024. na Timu ya Zimamoto wakiongoza mchezo huo kwa bao 1-0. Hadi mchezo iumamalizika Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
Mchezaji wa Timu ya New City  Joseph Mbaga akimpita beki wa Timu ya Zimamoto Amour Haji, wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar "PBZ Premier League 2023/2024, mchezo uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung.Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.