MAKAMU Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Msoud Othman, akizungunza na viongozi wa Mikoa , Ngome ya wazee , vijana na wanawake wa chama hicho pamoja na viongozi wampya wa ,matawi waliochaguliwa hivi karibuni. Mkutano huo umefanyika huko katika Ukumbi wa Majid Kiembesamaki wilaya ya Magharib ‘B’ Unguja leo tarehe 03.09.2023. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Baadhi ya Viongozi
wa Mikoa , Ngome ya wazee ,
vijana na wanawake pamoja na viongozi wampya wa
matawi waliochaguliwa hivi karibuni wa ACT Wazalendo wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo ambaye
pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Msoud Othman,
alipowahutubia katika mkutano wa viongozi hao uliofanyika huko katika Ukumbi wa
Majid Kiembesamaki wilaya ya Magharib ‘B’ Unguja leo tarehe 03.09.2023. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi
wa Mikoa , Ngome ya wazee ,
vijana na wanawake pamoja na viongozi wampya wa
matawi waliochaguliwa hivi karibuni wa ACT Wazalendo wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo ambaye
pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Msoud Othman,
alipowahutubia katika mkutano wa viongozi hao uliofanyika huko katika Ukumbi wa
Majid Kiembesamaki wilaya ya Magharib ‘B’ Unguja leo tarehe 03.09.2023. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar.
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman,
amewataka Viongozi wa Matawi wa Chama hicho waliochaguliwa kwenye uchaguzi
wa ndani wa hivi kuelewa kwamba wao ndio
msingi muhimu unaobeba dhima ya kuwapata
viongozi bora katika ngazi za majimbo, wilaya na mikoa wenye uwezo wa kusaidia
kujenga chama na kupata ufanisi mkubwa
ili kutimiza malengo ya chama hicho yaliyowekwa.
Mhe. Othman
ameyasema hayo huko ukumbi wa Majid Kiembesamaki Wilaya ya Magharib Unguja, alipozungumza na
viongozi mikoa, ngome za wanawake na
wazee, pamoja na Viongozi wapya wa Matawi ya chama hicho kutoka Mikoa yote ya
Unguja Kichama, kufuatia kukamilika
uchaguzi wa Viongozi wa matawi hivi karibuni.
Mhe. Othman
ambaye pia ni makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar , amefahamisha kwamba kuwepo
kwa viongozi hao makini pia ndio msingi madhubuti katika kujenga na kuimarisha
chama hicho ambao watasaidia kuendeleza
jitihada za kufanikisha maelngo na dhamira ya chama hicho ya kuwepo Zanzibar
yenye umoja na mshikamano wa kuiletea maendeleo Zanzibar.
Amefahamnisha
kwamba chama hicho kinahitaji viongozi makini watakosaidia jitihada za chama
hicho ya kuwepo Zanzibar moja na kuwataka kwenda kufanyakazi za kutumikia chama
kwa juhudi kuwa katika kutimiza maono ya chama hicho kwa kuzingatia uzalendo wa
kuipoenda nchi yao.
Aidha
amewataka viongozi hao waliochaguliwa kujenga mashirikio makubwa na uongozi wa ngome zote za chama hicho ili
kuweza kujenga taasisi imara itakayowezesha kukipatia ushindi chama hichi
katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025.
Mhe. Othman
amesema kwamba kufanyika kwa chaguzi hizo katika misimingi ya kidemokrasia ni
kelelezo muhimu kinaochonesha kwamba hakuna walikwenda kupanga safu kwa
kuwabeba baadhi ya wagombea lakini ni
wale waliofahamu wajibu na dhamira ya chama hicho ya kuijenga Zanzibar mpya.
Makamu
mwenyekiti huyo amewapongeza viongozi walichanguliwa na kuwataka kutokulala na
badala yake wafanye kazi kubwa ya kukitumikia chama sambamba na kuwashukuru
wagombea walioshindwa kwa kuonesha ukomavu na kwamba kushindwa kwao hakuoneshi
kwamba ni dhaifu kwa kuwa chama hicho kinahazi kubwa ya viongozi wengi wazuri katika kusimamia safu mbali
mbali.
Naye Naibu
Katibu Mkuu wa Chama hicho Zanzibar ambaye pia ni waziri wa Afya Afya Zanzibar
Mhe. Nassor Ahmed Mazrui amewataka vijana wa chama hicho kutorudi juma na
badala yake waendeleze umoja na msihakamano jutakaosaidia kupatikana mafanikio
ya chama na Zanzibar kwa jumla.
Kwa upande
wake Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Ismail Jussa Ladhu amewataka vijana
kuelewa kwamba wao ni tegemeo kubwa la maendeleo na umoja wa Zanzibar na kwamba
kuna haja ya kujifunza na kuelewa masuala mbali mbali yanayohusu historia ya
Zanzibar katika kusaidia ujenzi wan chi yao.
Mapema
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chama hicho Said Rashid Muhene amesema kwamba kazi ya
uchaguzi wa viongozi ngazi yay a matawi ya chama hicho unguja na Pemba
imefanyika kwa ufanisi mkubwa na kwanga
hivi karibuni utaendelea katika kuwapata vuiongozi wapya wa ngazi ya majimbo.
Kitengo cha
Habari ,
Ofisi ya
Makamu wa Kwanzawa wa Rais Zanzibar
Septemba
03, 2023.
No comments:
Post a Comment