Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli amewataka wanachama wa cha wakulima wa Ushirika wa Wakulima Wadogo Wadogo Kilimo cha Umwagiliaji Dakawa UWAWAKUDA katika skimu ya Dakawa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika kuboresha sekta ya umwagiliaji nchini ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji na uendelezaji.
Mhe. Judith Nguli ametoa kauli hiyo katika mkutano wa kawaida wa mwaka wa chama cha ushirika cha wakulima wa Umwagiliaji skimu ya Dakawa wilayani Mvomero mkoani Morogoro,ambapo mkutano huo ulihudhuriwa na wataalamu wa Tume ya Taifa Umwagiliaji makao makuu,pamoja na wataalamu ofisi ya Tume mkoa wa Morogoro.
Katika mkutano huo wataalamu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wametumia wasaa huo kutoa elimu ya umuhimu wa uchangiaji ada ya huduma za umwagiliaji na usajili wa chama cha umwagiliaji, sambamba na kueleza mpango wa serikali katika kuendeleza eneo la umwagiliaji katika skimu ya Dakawa.
"Moja kati ya vipengele ambavyo tunawaelimisha wakulima wetu waelewe kwamba miundombinu iliyopo ni ya kwao lakini pia wachangie ili serikali iweze kufikia malengo yake, kwani kwa sasa eneo linalofaa kwa umwagiliaji kwa nchi nzima ni hekta milioni 29 na eneo lililoendelezwa ni hekta 727,280, hivyo serikali ina majukumu na wakulima wana wajibu wa kuchangia ili serikali iweze kuboresha miundombinu iliyopo na kuiendeleza"
Kwa upande wake Mhandisi Umwagiliaji mkoa wa Morogoro Bw.Mohammed Mcheni, alibainisha kuwa skimu ya Dakawa ni miongoni mwa skimu kubwa katika mkoa huo ambapo takribani bilioni 23.4 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hiyo ambapo uzalishaji wake ni zaidi ya gunia 20 kwa ekari moja, hivyo serikali kuwekeza katika eneo hilo inaongeza usalama wa chakula kwa mkoa wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla.
“Eneo hili la Dakawa zipo hekta 1,000 ambazo hazijaendelezwa na zipo kwenye mpango wa mwaka huu wa fedha kufanya upembuzi yakinifu wa kina pamoja na kufanyia usanifu na tutazijenga hizo ambapo kukamika kwake kutakuwa na takribani hekari 8,000 ambazo zitatumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, kwahiyo serikali imedhamiria kuendeleza skimu ya Dakawa kwani ni eneo lenye uwezo mkubwa wa kuzalisha chakula cha kutosha"
Naye, afisa sheria Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bi. Magreth Shayo, ametoa wito kwa wakulima wa skimu ya Dakawa na wakulima wote nchini kuwa wakulima wapo katika mikono salama ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, kwani utekelezaji zoezi la uchangiaji ada ya huduma za umwagiliaji ni kwa mujibu wa wa sheria na ina manufaa kwa wakulima hivyo itasaidia kukuza sekta ya umwagiliaji nchini.
Aidha wakulima wameishukuru Tume kwa kuwapatia elimu ya sheria ya taifa ya umwagiliaji kwani awali walikuwa na uelewa mdogo juu ya sheria ya taifa ya umwagiliaji inayomtaka mkulima kuchangia ada ya huduma za umwagiliaji na kusajili chama chini ya Tume ya Umwagiliaji, hivyo ujio wa wataalamu hao umewasaidia kuwa na uelewa wa umuhimu wa zoezi hilo kwa manufaa ya sekta ya umwagiliaji nchini.
Skimu ya Dakawa ni skimu yenye ukubwa hekari 5016, ambapo serikali ipo mbioni kutekeleza mradi wa ujenzi bwala la umwagiliaji, ambalo litaongeza maji katika skimu hiyo ili kukabiliana na upungufu wa maji katika skimu hiyo na kuongeza uzalshaji wenye tija kwa wakulima wa Dakawa hivyo kuwa na
No comments:
Post a Comment