Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi ajumuika na waumini wa dini ya kiislamu katika Maulid viwanja vya Maisara

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu wa Zanzibar  Alhajj Balozi Seif Ali Iddi alipowasili katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, kuhudhuria Maadhimisho ya kusherehekea Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad  (S.A.W) yaliyofanyika jana usiku 27-9-2023 na (kushoto kwake) Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Hassan Othman Ngwali 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Sheikh.Alhabib Muhammad Bin Hussein Al-habshy kutoka Nchini Yemen, alipowasili katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, kuhudhuria Maadhimisho ya kusherehekea Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad  (S.A.W) yaliyofanyika jana usiku 27-9-2023 
WANAFUNZI wa Madrasasatul Fasbir Sabra Jamil kutoka Mbuzini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja wakisoma Qaswida ya Salamu ya Rais, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Maisara Wilaya Mjini Unguja Jijini Zanzibar kuhudhuria Maulidi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W ).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisoma ratiba ya Maadhimisho ya kusherehekea  Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika katika  viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar  jana usiku 27-9-2023, na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj Hemed Suleiman Abdulla na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar.Alhajj.Haroun Ali Suleiman na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Alhajj. Othman Masoud Othman.
VIONGOZI wa Dini na wageni waalikwa wakihudhuria katika Maulidi ya Maadhimisho ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana usiku 27-9-2023 katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja jana usiku 27-9-2023.
WAUMINI wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakihudhuria Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar  jana usiku 27-9-2023.
WAUMINI wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakihudhuria Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar  jana usiku 27-9-2023.
USTADHI Waziri Hakimu Ishaka akisoma Maulidi Barzanji Mlango wa Pili, wakati wa Maadhimisho ya Sherehe ya Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika katika viwanja vya Maisa Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja jana usiku 27-9-2023.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi katika kisimamo cha Qiyaam, wakati wa Maulidi ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja jana usiku 27-9-2023 na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Qasida ya Mwaka wa Kiislamu 1445 na Mshauri Mkuu wa Jumuiya ya Milade Nabii Association Zanzibar Sheikh. Sherali Champsi, wakati wa Maadhimisho ya Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana usiku 27-9-2023 katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar .
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na  Viongozi na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh,Saleh Omar Kabi (kushoto kwa Rais) na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman, baada ya kumalizika kwa Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja jana usiku 27-9-2023.
SHEIKH.Said Nassor Said kutoka Magogoni Unguja akisoma Dua ya Barzanji wakati wa Maulidi ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana usiku 27-9-2023 katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja.

WANAFUNZI wa Madrassatul Sufaiya kutoka Mwanakwerekwe Wilaya ya Mjini Unguja wakijumuika katika Maadhimisho ya Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika katika viwanja vya  Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja jana usiku 27-9-2023.
WANAFUNZI wa Jumuiya ya Maulidi ya Homu kutoka Mtaa wa Mtendeni Wilaya ya Mjini Unguja, wakisoma Maulidi ya Homu katika Maadhimisho ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman jana usiku 27-9-2023.
USTADH Omar Abdi Abdulla kutoka Ofisi ya Mufti Mkuu akisoma  Khutba ya Maadhimisho ya Maulidi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar jana usiku 27-9-2023.
WANAFUNZI wa Madrassatul Sanaa Muntakaa Kalam kutoka Ukongoroni Wilaya ya Kati Unguja wakisoma Qaswida, katika Maadhimisho ya Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja jana usiku 27-9-2023.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.