Habari za Punde

SMZ Imedhamiria Kurejesha Hamasa ya Mchezo wa Mpira Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imezamiria kwa dhati kurejesha hamasa za Mpira wa Zanzibar ili kuwafanya Vijana Kuwa nafasi moja ya ajira zao .

Hayo yamelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar , Ndg. Fatma Hamad Rajab Huko Katika Uwanja wa Mau Zedong mara baada ya kumaliza kwa mchezo wa Ngao ya Jamii Kati ya KMkM na JKU, katika mchezo huo Timu ya JKU imeshinda na kuondoa na Ushindi wa bao 5-2 dhidi ya KMKM katika mchezo9 wa Ngao ya Jamii mchezo uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung.

Amesema Serikali ya Awamu ya Nane imedhamiria hilo kuona mpira wa Zanzibar unakuwa bora kama miaka iliyopita .

Alisema kila Mtu anafahamu kuwa hivi sasa Wizara hiyo imejipanga kuhakikisha inatowa kila aina ya msada ili mpira huo unarudi katika jamii na kuwa fursa za Ajira kwa Vijana .

Katibu Mkuu Huyo Alifahamisha Kuwa Hivi Sasa Duniani Kote Mchezaji Wa Mpira Ndiyo Matajiri Wakubwa Hivyo Wakati Umefika Kwa Vijana Wa Zanzibar Kuchangamkia Fursa Hiyo Bila Ya Kujali Unatoka Sehemu Gani .

Alisema Katika Kuhakikisha Kuwa Mpira Huo Unakuwa Na Tija Wizara Kwa Kushirikiana Na Serikali Imekuwa Mstari Wa Mbele Katika Kuwatafuta Wadhamini  Na Tayari Pbz Imekuwa Mfano Kwa Kudhamini Ligi Kuu Na Azam Kwa Kuonesha Ligi Hizo Yote Ni Kujali Na Kuthamini Mpira Wa Zanzibar.

Mapema Katibu Huyo Amekabidhi Medali Kwa Jku Na Ngao Ya Jamii Ikiwa Ni Ishara Ya Kuanza Kwa Ligi Kuu Ya Zanzibar .

Nae Rais Wa Shirikisho La Mpira Zanzibar Suleiman Mahmoud Jabir amesema ZFF imejipanga kuhakikisha kuwa Ligi ya mwaka huu inakuwa Bora zaidi kwa vile Mfadhili mkubwa PBZ  imekuwa ni moja ya chachu ya maendeleo katika kuifadhili ligi hiyo .

Rais huyo ameishukuru Wizara ya Habari kwa kazi yao kubwa ya kuzungumza na Wafadhili ili kuja kuwekeza katika mpira wa Zanzibar .

Amesema katika kufikia malengo ya mpira wa Zanzibar wadau na wahisani wanatakiwa kuwa kitu kimoja kama malengo ya Serikali ya Awamu ya Nane ya kurejesha mpira katika hamasa yake .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.