Habari za Punde

Tanzania Kushiriki Mkutano wa KOAFEC – KOREA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, akizungumza na ujumbe wa Tanzania wakati wa kikao cha kukamilisha mapitio ya taarifa zitakazowasilishwa na Tanzania, katika mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, akimsikiliza Balozi wa Tanzania Jamhuri ya Korea Kusini Mheshimiwa Togolani Mavura, alipokuwa akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali wakati wa kikao cha kukamilisha mapitio ya taarifa zitakazowasilishwa na Tanzania, katika mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Amina Shaaban(kushoto), akitoa maelezo kuhusiana na ushiriki wa Tanzania mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine 54 za Afrika kushiriki mkutano huo Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Bw.. Aboud Mwinyi, akipitia taarifa mbalimbali wakati wa kikao cha kukamilisha mapitio ya taarifa zitakazowasilishwa na Tanzania, katika mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, akiongoza kikao cha ujumbe wa Tanzania kukamilisha mapitio ya taarifa zitakazowasilishwa katika mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, akisalimiana na Kamishna Idara ya Fedha za Nje Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, mara baada ya kupokelewa na ujumbe wa Tanzania katika Hoteli ya Ananti alipowasili kuongoza ujumbe huo kushiriki katika mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - WF, Busan, Jamhuri ya Korea Kusini)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.