Habari za Punde

ZHSF Wawataka Watoa Huduma za Afya Kupitia Vikosi vya Ulinzi na Usalama Kuboresha Huduma za Afya

 Na Rahma Khamis Maelezo             8/9/2023

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar Yassir Ameir Juma amewataka watoa huduma za Afya katika vituo vya  Vikosi vya Ulinzi na usalama  kubadilika  kutoa huduma bora zaidi.

 

 

"Tutowe huduma kwa moyo safi kwa kufata miongozo ya afya ili tusije kuvutana katika safari yetu tunayotaka kuianza," alisisitiza. Kaimu

 

Akifunga mafunzo ya kuwajengea uwelewa juu ya huduma bora kwa wananchi katika Ukumbi wa Michenzani Mall amesema wakati wanapotaka kutoa huduma bora kwa wananchi lazima kubadilika ili kuondoa malalamiko. 

 

Aidha amewasihi watoa huduma  hao wa  kuimarisha huduma  ya uhakika  kwa moyo wa kujitolea ili kuepusha migogoro kati ya wananchi na watoa huna hizo.

 

Amesema lazima watoa huduma wawe  wabunifu wa kubuni mbinu mbalimbali za kuwavutia wateja wao ikiwemo madakatari wao kujituma katika kazi, kuboresha majengo na kuwa na vifaa tiba vya kutosha.

 

"Wenzetu watoa huduma wa vituo binafsi wamejipanga kwa kila kitu kuhakikisha wanatoa huduma nzuri kwa wananchi vipi sisi tumejipanga je kuhusu hili," aliuliza Kaimu Mkurugenzi huyo.’’

 

Nae Afisa Mdhibiti  Ubora wa huduma za Afya Ahmed Saidi Moh’d amesema wanafanya mabadiliko ya sera ya afya kwa kuanzisha taasisi inayoshughulikia upatikanaji wa huduma bora  kwa wananchi wote  na kua endelevu.

 

Amesema huduma za afya zilikuwepo  tokea  awali lakini zilikua hazina viwango hinyo wamedhamiria kuziboresha zaidi huduma hizo ili ziweze kupatikana kwa  uhakika.

 

"Kuanzishwa kwa mfuko huu ni tija kwetu kwani tutakusanya fedha nyingi kulingana na kipato chetu, kupitia mfuko huu tutahakikisha zinakidhi kuhudumia wananchi wote wa Zanzibar" alisema.

 

Aidha amefahamisha kuwa kulingana na misingi ya kuanzishwa kwa mfumo huo  wameweza kugawa  makundi tofauti ya kusaidiana ikiwemo walemavu wagonjwa na waiojiweza.

 

Nao washiriki wa mafunzo hayo wameumba Mfuko huo  kusaidia hospitali ambazo zina upungufu wa vifaa jambo ambalo litasaidia kuondosha usumbufu kwa wananchi.

 

Wamesema wakati watakapopelekewa mikataba katika hospitali zao wapatiwe na orodha ya hospitali ambazo  zitatumia huduma hizo ili kuwaondeshea usumbufu wagonjwa.

 

Aidha wamefahamisha kuwa kupitia mafunzo hayo watahakikisha wanajiimarisha zaidi kwa kuweka vifaa vya kutosha ili kutoa huduma bora na kuitaka jamii kutumia fursa hiyo na kuacha kusikiliza maneno ya mitaani.

 

Mafunzo hayo  ya kuwajengea uwelewa juu ya Mfuko wa Huduma za Afya ni ya siku tatu na yameandaliwa na Watendaji wa Mfuko huo na kuwashirikisha watoa huduma katika Taassisi za Umma na Binafsi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.