Habari za Punde

Dk Hussein Mwinyi afungua kongamano la 24 la kimataifa la maji


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi mbalimbali alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Wilaya ya Mjini Unguja, Jijini Zanzibar kwa ajili ya ufunguzi wa Kongamano la 24 la Kimataifa la Maji, lililofanyika leo 25-10-2023 katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni  Zanzibar. 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akimsikiliza Dr.Joseph Mtamba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakati akitembelea maonesho ya Kimataifa ya Kongamano la Maji, katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar, kabla ya kulifungua Kongamano la 24 la Kimataifa la Maji, linalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Zanzibar leo 25-10-2023 na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa. 
WASHIRIKI wa Kongamano la 24 la Kimataifa  la Maji, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani)  akihutubia na kulifungua Kongamano hilo linalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar leo 25-10-2023.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Utafiti wa Maji  Afrika Kusini, Dr.Jennifer Molwantwa, wakati akitembelea maonesho katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Wilaya ya Mjini Unguja , kabla ya kulifungua Kongamano la 24 la Kimataifa la Maji, linalofanyika katika ukumbi wa hoteli hiyo leo 25-10-2023 na (kulia kwa Rais) Naibu Waziri Wizara ya Maji,Nishati na Madini Zanzibar Mhe. Shabaan Ali Othman.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kulifungua Kongamano la 24 la Kimataifa la Maji, linalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar  Wilaya ya Mjini Unguja leo 25-10-2023.(Picha na Ikulu) 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.