Habari za Punde

Michuano ya Ligi Kuu ya Zanzibar "PBZ Premier League 2023/2024. KVZ Yaitoa kileleni JKU kwa Ushindi wa Bao 3-0

Mshambuliaji wa Timu ya KVZ Akram Muhina akishangilia bao lake dhidi ya Timu ya JKU katika mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar "PBZ Premier League 2023/2024" na kuibika mchezaji bora wa mchezo huo, na kujinyakulia kitita cha fedha taslim shilingi laki mbili (200,000/=) zilizotolewa na Kampuni ya Emirate and Get 4 Less. Mchezo huo Timu ya KVZ imeshinda Bao 3-0 dhidi ya JKU mchezo uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.
Timu ya KVZ imekamata usukani wa Ligi Kuu Soka ya Zanzibar (PBZ Premier league) baada ya kuifunga JKU mabao 3-0 mchezo uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Mao Zedong.
Kwa matokeo hayo KVZ inaongoza Ligi hiyo ikiwa na alama 16 ikifuatiwa na JKU yenye points 13.
Licha ya kuongoza Ligi hiyo safu ya Ulinzi ya KVZ ndio safu bora mpaka sasa kwenye Ligi baada ya kucheza Michezo 6 mfululizo bila ya kuruhusu goli .
Wamecheza dakika 540 kwenye Ligi hiyo bila ya lango lao kufungwa goli hata la kuotea huku wao wakifunga Mabao 8 kwenye Michezo sita hiyo waliyocheza.
Msimu uliopita wa mwaka 2022-2023 KVZ ilikama nafasi ya pili kwenye Ligi hiyo huku KMKM ikitwaa Ubingwa huo.
Kwa kasi hii ya KVZ unaipa nafasi ya kutwaa ubingwa Msimu huu?


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.