Habari za Punde

Mhe Othman awasili Pemba kuanza ziara ya siku nne



Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Jumatano Oktoba 25, 2023 amewasili Kisiwani Pemba, kwa Ziara Maalum ya Siku 4, kwaajili ya Shughuli mbali mbali za Chama na Serikali.
Katika Uwanja wa Ndege wa hapa Pemba, Mheshimiwa Othman ambaye ameambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib, amepokelewa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya Siasa na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Baada ya kuwasili kisiwani Pemba, Mheshimiwa Othman amefika huko Pandani, Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini, ili kumjulia hali Mzee Masoud Juma Haji, pamoja na kufanya Mazungumzo Maalum na Wazee wa Kijijini hapo.
Kitengo cha Habari,
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,
Oktoba 25, 2023.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.