Habari za Punde

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mlezi wa CCM Mkoa wa Tanga Mhe.Hemed Seleiman Aendelea na Ziara Yake Wilaya ya Muheza na Pangani

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amewataka Viongozi na wanachama wa CCM Mkoa wa Tanga kuunganisha nguvu zao na kuwa na lengo moja la kushinda kwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika 2024.

Akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Pangani na Wilaya ya  Muhenza kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 amesema endapo Viongozi na  Wanachama wa CCM watakuwa wamoja katika kukitumikia, kukilinda na kutangaza mazuri yanayofanywa na CCM hakutakuwa na sababu itakayopelekea kukosa ushindi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa hata na Uchaguzi Mkuu ujao 2025.

Amefahamisha kuwa Mkoa wa Tanga umebahatika kuwa na Viongozi weledi na wachapa kazi ambao wamezidi kuimarisha mashirikiano  kati ya Chama na Serikali hatua ambayo inaashiriki kukipatia ushindi wa kishindo Chama cha Mapinduzi kwa nafasi zote kuanzia kata hadi Taifa.

Aidha amewasihi wale wote wanaotangaza nia ya kugombea nafasi mbali mbali za Uongozi katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 waache tabia hiyo na wasubiri wakati muafaka ufike ndipo watangaze nia zao kwani kufanya hivyo kwa sasa ni kukiuka kanuni na sheria za chama cha Mapinduzi

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amewataka Viongozi na wanachama wa CCM Mkoa wa Tanga kuunganisha nguvu zao na kuwa na lengo moja la kushinda kwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika 2024.

Akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Pangani na Wilaya ya  Muhenza kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 amesema endapo Viongozi na  Wanachama wa CCM watakuwa wamoja katika kukitumikia, kukilinda na kutangaza mazuri yanayofanywa na CCM hakutakuwa na sababu itakayopelekea kukosa ushindi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa hata na Uchaguzi Mkuu ujao 2025.

Amefahamisha kuwa Mkoa wa Tanga umebahatika kuwa na Viongozi weledi na wachapa kazi ambao wamezidi kuimarisha mashirikiano  kati ya Chama na Serikali hatua ambayo inaashiriki kukipatia ushindi wa kishindo Chama cha Mapinduzi kwa nafasi zote kuanzia kata hadi Taifa.

Aidha amewasihi wale wote wanaotangaza nia ya kugombea nafasi mbali mbali za Uongozi katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 waache tabia hiyo na wasubiri wakati muafaka ufike ndipo watangaze nia zao kwani kufanya hivyo kwa sasa ni kukiuka kanuni na sheria za chama cha Mapinduzi.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuulinda Muungano kwa juhudi zote ili uendelee kuwaunganisha Watanzania na yoyote atakaejaribu kuharibu taswira ya muungano huo atawajibishwa kwa mujibu wa Sheria. 

Nae Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ndg.  Rajab Abdulrahman Abdulla amemuhakikishia Mlezi wa CCM Mkoa wa Tanga kuwa ataisimamia vyema Miradi inayotekelezwa na Serikali kwa kuhakikisha inajengwa katika viwango vyenye ubora wa hali ya juu na kutoa onyo kwa wasimamizi wa miradi hiyo kuwa CCM Mkoa wa Tanga haitamvumilia yoyote atakaefanya ubadhirifu wa fedha na vifaa vya ujenzi wa  miradi hiyo. 

Amefafanua kuwa kuwapatia maendeleo wananchi ndiko kunakowapelekea kuwa na imani na CCM na Serikali kwa ujumla hivyo, umakini na uwajibikaji kwa Viongozi wa ngazi zote za chama na serikali kutaleta matokeo chanya katika chaguzi zote nchini. 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe. Zainab Abdalla amemshukuru Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa miradi mbali mbali ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa katika Mkoa wa Tanga ambayo itatatua kero mbali mbali za wananchi. 

Amemuahidi Mlezi huyo kuwa kutokana na miradi iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita hakuna sababu ya CCM kushinda katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na Uchaguzi wa Dola mwaka 2025.

Imetolewa na itengo cha Habari (OMPR)

10/10/2023

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.