27
Oktaba, 2023
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na waumini wa Kiislamu kwenye Ibada ya Sala ya
Ijumaa, viwanja vya Markaz Bungi, Wilaya
ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Alhaj Dk.
Mwinyi aliendelea kuikumbusha jamii juu ya kuamrishana mema na kukatazana maovu
ili kuendelea kupata radhi za Mwenyezi Mungu (S.W) na taifa lenye maadili na kumcha
Mungu.
Alisema, viongozi
wa dini wananafasi kubwa kwa jamii kuwaelekeza mambo ya heri ili kupata jamii
yenye busara, upendo, amani, umoja na mshikamano na kuongeza kuwa kupitia
utengamano huo hata Serikali inapata fursa nzuri ya kuwaletea maendelo ya watu
wake kwa ufanisi wa hali ya juu.
Alhaj Dk.
Mwinyi aliwaeleza waumini hao kwamba, bado jamii inahitaji msaada mkubwa wa
viongozi wa dini ili kurekebisha mitazamo ya waovu wachache, kwa kuyakataza na
kuyakemea maovu yanayotendeka kupitia kundi la vijana ambao ni waathirika wakubwa
kwenye suala la mporomoko wa maadili.
Alisema, viongozi hao wanamchango mkubwa kwa Serikali hususani
kwenye suala zima la kujenga maadili ya umoja wa watu, suala ambalo linaleta mazingira
mazuri ya maendeleo.
Sambamba na
kuwaomba viongozi wa dini na waumini hao kuendelea kuliombea dua taifa na
viongozi wake kupitia kazi kubwa wanayoifanya ya kulitumikia taifa.
“Sisi viongozi tunahitaji dua zenu kuombewa ili kutimiza
majukumu yetu kwa ufanisi mkubwa” Alisisitiza Alhaj Dk. Mwinyi.
Naye, Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar, Sheikh
Khalid Ali Mfaume, alipongeza juhudi za masheikh wa tablikh kwa
kufanikisha majukumu yao kwa uadilifu mkubwa bila kuchanganya siasa na
mikinzano isiyofaa kwa jamii, pia aliwaomba mashekh hao kuendelea kuwaombea Rais
Alhaj Dk. Mwinyi na viongozi wa nchi kwa
kazi kubwa wanayoifanya ya kulitumikia taifa.
Akizungumzia
umuhimu wa darsa za kufundishana mambo mema ya heri, Khatib wa sala ya Ijumaa viwanjani
hapo Sheikh, Abubakar Mubarak, aliwaeleza waumini kwenye mkusanyiko huo na jamii
kwa ujumla kwamba darsa za kiislamu hukusanya waumini wa chache kwenye eneo
moja lakini kwenye mkusanyiko mkubwa kama huo uliokusanya miji, nchi na
makabila tofauti yasiyojuana kukaa pamoja na kumtaja Allah (S.W) hupatikana
zaidi radhi za Mwenyezi Mungu.
IDARA YA
MAWASILIANO IKULU, ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment