Habari za Punde

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan akutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje ya India

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje ya India Mhe. Dkt. Subrahmanyam Jaishankar aliyeambatana na ujumbe wake mara baada ya kuwasili New Delhi kwa ajili ya ziara ya Kitaifa.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje ya India Mhe. Dkt. Subrahmanyam Jaishankar mara baada ya mazungumzo New Delhi nchini humo tarehe 08 Oktoba, 2023. Wengine pichani ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba, Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba pamoja na Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Anisa Mbega wa kwanza kulia.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.