Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadid Rashid akizungumza na wazazi,walezi na wanafunzi kuhusu uwepo wa Vitendo vya Udhalilishaji huko Skuli ya Bambi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Wazazi,Walezi na Wanafunzi wakisikiliza kwa makini nasaha kuhusu vitendo vya udhalilishaji kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadid Rashid (hayupo pichani) huko Skuli ya Bambi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR
Na Fauzia Mussa, Maelezo
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadid Rashid amewataka Walezi kushirikiana na Walimu ili kuondokana na vitendo vya udhalilishaji.
Akizungumza na wazazi,walezi,walimu na wanafunzi huko Skuli ya Bambi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja amesema vitendo hivyo vimekua vikigharimu na kukatisha malengo ya watoto hao siku hadi siku.
Alisema jukumu la kupinga vitendo vya udhalilishaji si la Serikali pekee bali jitahada za pamoja zinahitajika ili kutokomeza vitendo hivyo.
“kila mmoja ni mchunga na ataulizwa juuu ya alicokichunga” alinukuu Mkuu huyo
Aidha aliwataka Walezi kusimamia vyema maelezi ya watoto wao ili kuwakinga na vitendo hivyo kwani endapo watawaachia walimu pekee tatizo hilo litakua endelevu.
Alifahamisha kuwa endapao jamii itaacha vitendo vya udhalilishasji vitawale kuna hatari ya kukosa viongozi shupavu wa baadae.
“ tukiicha hali hii iendelee hatutakua na mashehe,viongozi wala walimu katika nchi yetu”alifahamisha Mkuu huyo.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Kati Marina Thomas amewataka wazazi kukaa karibu na watoto wao na kufatilia nyendo zao kwa kuwadadisi ili kuweza kugundua uwepo wa vitendo hivyo katika hatua za awali.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu Skuli ya Msingi Bambi Muhammed Ramadhan Mapuri amewaomba Walezi kuwachunga watoto wao kutokana na vikundi vya madawa ya kulevya kwani kunachangia uwepo wa vitendo vya ubakaji,udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia.
No comments:
Post a Comment