Habari za Punde

Riziki Pembe akagua ujenzi wa Dakhalia Skuli ya Chwaka, Tumbe kisiwani Pemba


 Wanafunzi wametakiwa kuongeza bidii katika Masomo yao ili waweze kupata viwango Bora vya Ufaulu.
Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Kamati Tekekelezaji ya Baraza Kuu la UWT Taifa Mh. Riziki Pembe Juma wakati akizungumza na Walimu na Wanafunzi wa Skuli ya Chwaka Tumbe Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba mara baada ya kukagua ujenzi wa Daghalia katika Skuli hiyo.
Mh. Riziki amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawekeza Fedha nyingi katika Sekta ya Elimu ili kuwawezesha Wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki hivyo amewataka Wanafunzi kutumia vyema fursa hiyo kwa kuongeza juhudi katika Masomo yao.
Mjumbe huyo wa Kamati Tekelezaji ya Baraza Kuu la UWT ambae pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amewataka Wanafunzi kujiepusha na Vitendo vya Udhalilishaji kwa kutokubali kushawishiwa.
Aidha Mh. Riziki amewataka Walimu kuongeza bidii katika Ufundishaji ili kutimiza ndoto za Wanafunzi katika Maisha yao.
Nae Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mwalimu Moh'd Nassor Salim amesema Ujenzi wa Daghalia ya Wanawake katika Skuli hiyo ni miongoni mwa jitihada zinazofanywa na SMZ katika kuongeza Ufaulu na kufuta divisheni sifuri.
Amelishukuru Shirika la KOICA kupitia KFHI kwa kusaidia ujenzi wa Daghalia inayotajiwa kuchukua kukaa Wanafunzi 80 kwa wakati mmoja.
Akisoma Risala kwa Niaba ya Walimu na Wanafunzi wa Skuli ya Chwaka Tumbe Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo Khatibu Rashid Mwinyi ametaja changamoto mbali mbali ikiwemo kutokuwepo kwa uzio katika Daghalia hiyo ya Wanawake.
Wakati huohuo Mjumbe Wa Kamati Tekekelezaji ya Baraza Kuu la UWT Taifa amekabidhi Msaada wa Chakula kwa Wanafunzi wanaokaa kambi ya Matayarisho ya Mtihani katika Skuli ya Chwaka Tumbe.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.