Habari za Punde

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe.Dkt Tulia Ashiriki Mkutano wa Jumuiya ya Madola Nchini Ghana

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa kwanza kulia), akifuatilia Mkutano wa 66 wa Bunge la Jumuiya ya Madola (CPC) unaoendelea katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Accra nchini Ghana,(kulia kwake) Mhe. Abdallah Mwinyi, Mhe. Dkt. Alice Kaijage na Mhe. Dkt. Pius Chaya.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 5 Oktoba, 2023 ameshiriki Mkutano wa 66 wa Kibunge wa Jumuiya ya Madola (CPC) unaoendelea katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Accra nchini Ghana wenye dhima isemayo “The Commonwealth Charter 10 years on: Values and Principles for Parliaments to Uphold”

Katika Mkutano huo, Dkt. Tulia ameambatana na baadhi ya Wabunge akiwemo Mhe. Dkt. Alice Kaijage, Mhe. Abdallah Mwinyi, Mhe. Dkt. Pius Chaya, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama, Mhe. Elibariki Kingu pamoja na Katibu wa Bunge Bi. Nenelwa Mwihambi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.