Habari za Punde

Matembezi wa Vijana wa UVCCM Yakiendelea Pemba Katika Mkoa wa Kaskazini Pemba

MWENYEKITI wa UVCCM taifa Mohamed Ali Kawaida pamoja na  Kiongozi Mkuu wa Matembezi Machano Ali Machano na Maafisa usafirishaji wakiendesha pikipiki za bodaboda mara baada ya kuzungumza nao ikiwa ni ishara ya ushirikiano na kuadhimisha miaka 60 Mapinduzi ya Zanzibar.
MWENYEKITI wa UVCCM taifa Mohamed Ali Kawaida,Kiongozi Mkuu wa Matembezi Machano Ali Machano,Mbunge wa Viti Maalum wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe.Munira Mustafa Khatib(kushoto wa pili),Mwakilishi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mhe.Hudhaima Mbarouk Tahiri(wa kwanza kushoto) na Mwenyekiti wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Hashir Ali wakigawa vazi maalum la kuwatambulisha Maafisa usafirishaji wakati wa utekelezaji wa majukumu yao(Refrectors).

Na.Is-Haka Omar - Pemba.

KIONGOZI Mkuu wa Matembezi ya UVCCM ya kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar Machano Ali Machano ,amewasihi Maafisa Usafirishaji(bodaboda) wa Mkoa wa Kaskazini Pemba kuwa makini wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ili kupunguza ajali.


Hayo ameyasema wakati akizungumza na kusikiliza changamoto za bodaboda katika Matembezi hayo Pemba.


Machano,alisema umakini ndio nyenzo pekee ya kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi kwa ufanisi.


Alisema kuwa UVCCM ina dhamana kubwa ya kuyasemea makundi mbalimbali ya vijana ili changamoto zao zitafutiwe ufumbuzi na taasisi husika.


Katika maelezo yake,Mkuu huyo wa Matembezi alisema Serikali ya awamu ya nane chini ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi,inaendelea kutoa fursa za mikopo yenye masharti nafuu hivyo kundi hilo wafuate utaratibu na UVCCM itawasemea kuhakikisha wananufaika na mikopo hiyo.


“Matembezi ya kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ni jukwaa la kutuunganisha vijana wa makundi mbalimbali kukaa pamoja na kujadiliana kwa kina mafanikio na changamoto mbalimbali zinazotukabili ili kupata namna bora ya kuzitatua

 

”UVCCM tutaendelea kuwasemea mema pamoja na kuhakikisha asilimia za fedha zinazotengwa na Serikali kwa ajili ya uwezeshaji wa kundi la vijana kutoka Mabaraza ya Manispaa na Halmashauri zinawanufaisha nyinyi katika kupata mitaji na kujikwamua kiuchumi,alisema Machano.

 

Machano, ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki amelitaka kundi hilo la Maafisa usafirishaji kujiepusha na vitendo vya matumizi ya dawa za kulevya,udhalilishaji wa kijinsia na ukabaji  badala yake waendelee kuwa waaminifu katika utekelezaji wa majukumu yao.

 

Naye Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mohamed Ali Kawaida,alisema aliwapongeza Maafisa usafirishaji hao kwa kazi kubwa wanayofanya ya kutoa huduma za usafiri kwa wananchi wa makundi mbalimbali.

 

Kupitia kikao hicho Mkuu huyo wa Matembezi Machano Ali na Mwenyekiti wa UVCCM taifa Mohamed Kawaida pamoja na Viongozi mbalimbali wa UVCCM wa Mkoa wa Kaskazini Pemba,waligawa mavazi maalum ya kuwasadia kutambulika kwa urahisi wakati wa utendaji wa kazi zao hasa usiku(Reflectors)kwa Maafisa wote wa Usafirishaji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.