Habari za Punde

Waandishi wa Habari, Wtendaji wa Afya na Idara ya Mifugo Wajengewa Uelewa wa Usugu wa Vimelea vya Maradhi Dhidi ya Dawa Zanzibar

Mratibu wa usugu wa Vimelea vya maradhi  Wizara ya Afya Zanzibar Muhidin Omar akiwasilisha mada ya usugu wa vimelea vya  maradhi dhidi yadawa  kwa Waandishi wa  habari wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa yaliofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.

Na Imani Mtumwa,   Maelezo

Mratibu wa Usugu wa Vimelea vya Maradhi Wizara ya Afya Dk. Muhidini Omar ameitaka jamii kutumia Dawa kwa  usahihi ili kupunguza ongozeko la Maradhi katika jamii.

Akizungumza wakati akitoa Mafunzo kwa Waaandishi wa habari  juu ya Usugu  wa Vimelea dhidi ya Dawa katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo amesema jamii imezowea  kutumia dawa bila ya kuonana na Daktari jambo ambalo linapelekea kuharibu Afya za Wananchi.

Akifafanua kuhusu  dhana ya Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa alisema ni pale dawa zilizokuwa zikitumika awali kushindwa kutibu Maradhi ya kuambukiza kama vile Kifua kikuu, Nimonia na Ukimwi .

Hata hivyo alisema miongoni mwa visababishi vya usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa ni pamoja na mazingira ni ukataji miti ovyo na muingiliano wa watu hupelekea kuengezeka kwa Maradhi.

Aidha alisema kwa Zanzibar asilimia 90 ya vimelea vimeonyesha Usugu dhidi ya Dawa ambazo zinatumika kutibu maradhi mbali mbali kwa uzembe hivyo aliisisitiza jamii kutumia dawa kwa kuzingatia maelekezo ya daktari ikiwemo kukamilisha  dozi ili kupunguza ongezeko la vifo katika nchi yetu.

Kwa upande wake Daktari Mkuu wa Mifugo Idara ya Mifugo Zanzibar Dr Ali Zahran amesema miongoni mwa sababu kubwa zinazochangia usugu wa vimelea dhidi ya maradhi  ni pamoja na Wanyama kwani wafugaji hawataki kufuata ushauri wa daktari katika kuwatibu wanyama  jambo ambalo linapelekea kwa Usugu wa Maradhi.

Alifahamisha Serikali imeweka  vituo 11 vya kutibu wanyama  na vituo zaidi ya 10 binafsi hivyo amewataka  wafugaji na wakulima kuvitumia vituo hivyo ili kulima na  kufuga kiutalamu ili kumlinda Mtumiaji.

Kwa upande wao Washiriki wa Mafunzo hayo wamesema wataifanyia kazi Elimu hiyo kwa   kutoa taarifa  na kufanya vipindi mbali mbali  vinavyohusiana na usugu wa vimelea dhidi ya dawa kwa jamii ili  ipate kuelimika juu ya tatizo hilo.

Hata hivyo wameitaka Wizara ya Afya na Wizara ya Kilimo na Mifugo kushirikiana vyema na Waandishi wa Habari ili kuhakikisha tatizo hili linaloikumba jamii linapungua kwa wananchi kwa kuwapatia elimu yakutosha ili kupunguza Maradhi na Vifo.

Mafunzo hayo ya siku moja  yaliwashirikisha Waandishi wa Habari,Wataalamu wa Afya,na pamoja na wataalamu kutoka Idara ya  Mifugo Zanzibar.

 

Mwandishi wa habari wa Gazeti la kiengereza la Daily News Issa Yussuf akichangia mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari juu ya usugu wa  vimelea vya  maradhi  dhidi ya dawa yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.
Mwandishi wa habari wa Zanzibar Cable Malik Shaharan akichangia  mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari juu ya usugu wa vimelea vya maradhi dhidi ya dawa   yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.
Afisa Habari kutoka Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Mwantanga Juma akichangia mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari juu ya usugu wa  vimelea vya  maradhi  dhidi ya  dawa  yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.

Mwandishi wa habari wa ZBC Radio Hinja Pongwa akichangia mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari juu ya usugu wa  vimelea vya maradhi dhidi ya dawa  yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.