Habari za Punde

Waandishi Watakiwa Usalama Wao Kwanza

Na Issa Mwadangala

Jeshi la Polisi Mkoani Songwe limewataka waandishi wa habari kujali usalama wao pindi  wanapotekeleza majukumu yao ya kutafuta habari na kuuhabarisha Umma.

Hayo yamesemwa Desemba 05, 2023 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP Theopista Mallya wakati wa mdahalo wa awamu ya pili ya majadiliano kati ya Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe na Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na Waandishi wa habari mkoani humo.

“Waandishi wa habari ni vyema kuzingatia usalama wako kwanza wakati unatekeleza majukumu yako ya kukusanya taarifa sehemu zenye vurugu au sehemu nyingine ni bora kujiangalia wewe kwanza na sio kuhatarisha maisha yako katika mazingira hatarishi ambayo yanaweza kukusababishia madhara ambayo unaweza kuyaepuka” Alisema.

Kamanda Mallya Alihitimisha kwa kuwasihi waandishi wa habari kujikita katika kujielimisha kitaaluma na kujua mipaka ya kazi yao pindi wanapotimiza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa jamii juu ya uhalifu kwa njia ya  mtandao ili jamii ipate kuelewa.

Kwa upande wa waandishi wa habari wamelishukuru Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe kwa elimu waliyoipata na wamemuomba Kamanda Mallya kuendeleza kudumisha ushirikiano uliopo kati yao na Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.