Habari za Punde

OFISI YA MSAJILI WA HAZINA WAKAA PAMOJA NA TAASISI ZA UWEKEZAJI WA UMMA KUIMARISHA UTENDAJI

Msaji wa hazina wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Waheed Ibrahim Sanya  akifungua kikao kazi na wakuu wa taasisi za uwekezaji za umma huko ukumbi wa Zura Maisara mjini Unguja.

Na Rahma Khamis Maelezo

Msajili wa Hazina wa Selirikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  Waheed Ibrahim Muhammed Sanya amewataka watendaji wa Taasisi mbalimbali na mashirika ya umma kushirikiana na Ofisi hiyo ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi.

 

Akifungua mkutano wa kuwajengea uwelewa watendaji Wakuu wa Taasisi za Uwekezaji wa Umma katika Ukumbi wa Zura Maisara amesema kikao hicho kitawawezesha kufahamu majukumu yao pamoja na kujua Ofisi ofisi ya msajili wa hazina ina nafasi  gani katika utendaji wao.

 

Amesema Taasisi ya hazina ni Taasisi kubwa inayofanya  kazi kwa karibu na taasisi nyingi za Serikali hasa zinazozalisha hivyo ni wajibu wao kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo nchini.

 

Amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kujenga uelewa kwa watendaji wa taasisi hizo juu ya kazi zinazofanya na ofisi ya msajili wa hazina  pamoja na kuwapatia fursa ya kuwasilisha changamoto zinazowakabili katika taasisi zao na kuzipatia ufumbuzi .

 

Aidha amefahamisha kuwa  ofisi hiyo ina mpango wa kuwapatia  mafunzo ya muongozo kwa baadhi ya  watendaji iili kuwajengea uwezo na kuleta mabadiliko chanya katika Taasisi zao.

 

“Endapo watendaji  wakuu wa taasisi hizi watakua na uelewa mzuri juu ya ofisi hii wataweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kuwa mabalozi wazuri kwa wanaoowaongoza”alisema Sanya

 

Akiwasilisha mada ya mahusiano baina ya ofisi na mashirika ya umma na mpango kazi wa ofisi hiyo Kaimu Mkuu wa Mashirika ya Uwekezaji ya Umma CPA Mussa Ali Juma amesema kuwa Serikali inatoa gawio kwa taasisi zake  kupitia uchangiaji wa Taasisi hizo ili kuendeleza utendaji kazi wao na kuletaa maslahi kwa jamii na taifa kwa ujumla.

 

Akitoa ufafanuzi kuhusu ofisi ya Msajili wa hazina Mussa amesema kuwa kuna haja ya kufanya muongozo  mmoja katika Taasisi kutokana ma uwepo wa miundo tofauti katika Taasisi hizo.

 

Amesmea lengo ni kuona taasisi hizo zinafanya uwekezaji mzuri kwa maslahi ya Taifa kwani ndio wernye jukumu la kutoa muongozo na kusimamia mali za umma katika taasisi  hizo.

 

Ameongeza kuwa Kazi yake kubwa  ni kuruhusu kutumia au kuondolewa kwa mali za umma pamoja na  kutoa muongozo utakaoelekeza namna nzuri ya kuongoza taasisi zao

 

Nao washiriki wa mkutano huo wameahidi kutoa ushirikiano wao katika Ofisi hiyo sambamba na kukubaliana katika utendaji wa wa kazi zao.

 

Aidha wanaomba kufahamu mikataba wanayoingia na Taasisi nyengine ili kujua muongozo husika wanaotakiwa kuutumia katika kazi zao.

 

Wameongeza kuwa ofisi ya msajili wa hazina kuweke muongozo maalumu kwa Taasisi zinazojiendesha kibiashara ili kuondosha changamoto zinazoweza kujitokeza na kuleta tija.

 

Mkutano huo umeshirikisha Taasisi mbalimbali za kibiashara ikiwemo ZSTC, ZMUX,ZAWA, ZAFICO,Shirika la magazeti na Shirika la utangazaji na Shirika la  Bandari . 

Kaimu mkuu wa mashirika ya uwekezaji wa umma CPA Mussa Ali Juma akiwasilisha maelezo kuhusiana na ofisi ya  msajili wa hazina,mahusiano baina ya ofisi na mashirika ya umma na mpango kazi wa ofisi hiyo katika kikao kazi kilichofanyika ukumbi wa Zura Maisara mjini Unguja.
Baadhi ya wakuu wa wa taasisi za uwekezaji za umma wakiwa katika kikao kazi kilichoandaliwa na ofisi ya msajili wa hazina kilichofanyika ukumbi wa Zura Maisara mjini Unguja.
Kaimu  Mkurugenzi mkuu  mfuko wa huduma za afya (ZHSF) Yaasin Ameir Juma akichangia katika kikao kazi baina ya  Ofisi ya msajili wa hazina na wakuu wa taasisi za uwekezaji za umma kilichofanyika ukumbi wa Zura Maisara mjini Unguja.
Mhariri mtendaji shirika la magazeti ya Serikali Ali Haji Madini akichangia katika kikao kazi baina ya  Ofisi ya msajili wa hazina na wakuu wa taasisi za uwekezaji za umma kilichofanyika ukumbi wa Zura Maisara mjini Unguja.
Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya maji (ZAWA) dkt. Salha akichangia katika kikao kazi baina ya  Ofisi ya msajili wa hazina na wakuu wa taasisi za uwekezaji za umma kilichofanyika ukumbi wa Zura Maisara mjini Unguja.
Mkurugenzi mtendaji Shirika la Bandari Zanzibar Akfal Khamis akichangia katika kikao kazi baina ya  Ofisi ya msajili wa hazina na wakuu wa taasisi za uwekezaji za umma kilichofanyika ukumbi wa Zura Maisara mjini Unguja.

Mkugenzi Mkuu shirika la utangazaji (ZBC) Ramadhan Bukini akichangia katika kikao kazi baina ya  Ofisi ya msajili wa hazina na wakuu wa taasisi za uwekezaji za umma kilichofanyika ukumbi wa Zura Maisara mjini Unguja.

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.