Habari za Punde

ZOI yawataka Wazazi na Walezi kuwasomesha lugha Watoto wao.

 Na Takdir Ali, Maelezo. 15/02/2024.

 Uongozi wa Kituo kinachotoa elimu Zanzibar (ZOI) umeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuwapatia elimu kwa Wananchi ili kuweza kufuta ujinga na kujiajiri au kuajiriwa.

 

Hayo yameeleze na Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi hiyo Kassim Suliman Ushanga wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari huko Ofisini kwake Amani Bopar Wialaya ya Mjini.

 

Amesema iwapo Wananchi watajifunza lugha za kigeni wataweza kupata ajira katika sehemu mbalimbali ikiwemo hoteli jambo ambalo litaweza kuwapatia kipato cha kuendesha Maisha yao ya kila siku.

 

Aidha amesema lugha za kigeni, zitawawezesha Wananchi kufanya mawasiliano kwa Taasisi mbalimbali na kuweza kupata ajira na kuondokana na hali tegemezi katika familia na jamii kwa Ujumla.

 

Mbali na hayo amewaomba Wazazi na Walezi kuwapeleka Watoto wao waliomaliza masomo katika vyuo, vinavyotua mafunzo ya lugha za kigeni ili waweze kupata ajira na kuepuka kujiingiza katika vitendo viovu ikiwemo Udhalilishaji,wa kijinsia, Utumiaji wa dawa za kulevya na Bangi.

 

Kituo cha ZOI, kinatoa Mafunzo mbalimbali ikiwemo lugha tofauti za kigeni, darasa la Watu wazima wasiojuwa kusoma na kuandika pamoja na fani za Kopyuta ili kuisaidia jamii na Serikali katika kupiga vita aduwi Ujinga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.