Habari za Punde

JUMUIYA YA MAENDDELEO YAFARIJI WATOTO WENYE ULEMAVU MAKUNDUCHI

Mkuu wa Wilaya ya kusini Galos Nyimbo  akikabidhi sare za skuli Kwa wanafunzi mbalimbali wenye mahitaji maalum katika Wilaya hiyo, ambao ni msaada uliotolewa na Jumuiya ya Makunduchi Devolopment Organisation huko Ofisini kwake Makunduchi Wilaya ya Kusini.

Na Takdir Ali. Maelezo. 21.03.2024.

Mkuu wa Wilaya ya Kusini Galos Nyimbo ameipongeza Jumuiya ya Makunduchi Devolopment Organisation kwa kutoa msaada wa sare za Skuli na viti vya maringi 3 kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Jimbo la Makunduchi.

Pongezi hizo amezitoa huko Ofisi kwake Makunduchi wakati alipokuwa akikabidhi msaada huo kwa Wanafunzi wa Skuli 5, wenye mahitaji katika Jimbo hilo.

Amesema Watoto hao wanahitaji misaada ya hali na mali hivyo Serikali ya Wilaya ya kusini inaunga Mkono juhudi zinazochukuliwa na Jumuiya hiyo katika kuunga mkono juhudi za Serikali Kuwapatia elimu bora Wananchi.

‘‘Kuna Taasisi nyingi zinatoa misaada katika masuala ya michezo lakini hawaelekezi zaidi kwa Watoto kama hawa hivyo kitendo mulichofanya ni cha kupigiwa mfano na mimi kama Mkuu wa Wilaya ya kusini naahidi tutakuwa bega kwa bega. Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Amesema Watoto wenye mahitaji maalum wanauwezo wa hali ya juu hivyo wakiunganishwa na kupatiwa elimu wataweza kuwa wataalamu wazuri wa hapo baadae.

Amefahamisha kuwa Serikali imeweka mazingira bora ya kusomea kwa Watu hao katika vyuo vikuu hivyo amewataka Watoto hao kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza malengo yao ya kupata elimu.

Hata hivyo amewataka Waalimu kuwa na moyo mkunjufu na kuwapenda Wanafunzi hao ili waweze kupata rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu sambamba na kuwaomba Wazazi na Walezi kufuatilia nyendo za Watoto wao ili kuweza kuwakinga na matatizo mbalimbali ikiwemo ya Udhalilishaji.

Kwa uapnde wake Afisa elimu Wilaya ya Kusini Mussa Nahodha Makame amewataka Viongozi wa Jumuiya Makunduchi Devolopment Organisation kuendelea kutafuta misaada ya hali na mali ili waweze kuwapatia Watoto wenye mahitaji maalum.

Hata hivyo ameomba msaada huo kuwa endelevu na usiishie Skuli za Makunduchi pekee kwani katika Wilaya hiyo kumekuwa na Watoto wengi wa aina hiyo wanaohitaji misaada.

Nao baadhi ya Wazazi na Walezi wa Watoto wenye mahitaji maalum ambao wamekabidhiwa msaada huo wamesema umekuja wakati muafaka kwani baadhi ya ya Watoto wanashindwa kuende Skuli kutokana na ukosefu wa vigari vya kutembelea.                                 

Jumuiya ya Makunduchi Devolopment Organization imekabidhi sare za Skuli kwa Wanafunzi 90 na Baskeli 5 za Maringi 3 kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum, kwa 5 za Jimbo la Makunduchi ikiwemo Skuli ya Mtende, Mialeni, Kiungoni, Kusini na Makunduchi.

Mkuu wa Wilaya ya kusini Galos Nyimbo akizungumza na walimu na wanafunzi wa Watoto wenye mahitaji maalum wakati wa zoezi la ugawaji wa sare za skuli kwa wanafunzi hao, iliotolewa na Makunduchi Devolopment Organisation, lililofanyika Ofisini kwake  Makunduchi Wilaya ya Kusini.

Afisa Elimu Wilaya ya kusini Mussa Nahodha Makame  akitoa neno la shukrani katika hafla ya ugawaji wa sare kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, ambao ni Msaada wa Jumuiya ya Makunduchi Devolopment Organization huko Ofisi ya mkuu wa Wilaya  Makunduchi Wialaya ya Kusini.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya maendeleo ya Makunduchi Mwazini Jogoo akitoa maelezo mafupi wakati wa ugavi wa sare za skuli kwa wanafunzi wenye Mahitaji maalum ikiwa ni Msaada kutoka Jumuiya ya Makunduchi Devolopment Organisation huko Ofisi ya Mkuu wa Wilaya  Makunduchi Wialaya ya Kusini.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.