Habari za Punde

Miembeni Yaibuka Mabingwa Kombeb la Masauni &Jazeera Cup 2023/2024 * Masauni Apania Kuimarisha Michezo Jimboni


Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Hamad Masauni akimfisha medali nahodha wa timu ya Kikwajuni Yunus Benard Moshi.Timu yao imechukua nafasi ya Pili wa Kombe la Masauni &Jazeera Cup katika mchezo wa Fainali uliofanyika katika Uwanja wa KMKM Maisara Unguja. 

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Yussuf Masauni ataendelea kuchukua juhudi mbalimbali za kuhakikisha anaimarisha sekta ya  michezo ili kuwa ni sehemu ya ajira kwa vijana wa Jimbo hilo

Waziri Masauni ameeleza hayo wakati wa fainali ya Ligi ya Masauni & Jazeera Cup iliyowakutanisha timu ya Miembeni na Kikwajuni katika dimba la uwanja wa KMKM Maisara Mjini Unguja

Katika fainali hiyo timu ya  Miembeni imeiadhibu kichapo cha bao 5 - 2 Dhidi ya Kikwajuni

Masauni amesema ni dhahiri kuwa ligi hiyi imekua chachu ya vijana kuonekana na kupata ajira rasmi kupitia vilabu vikubwa hapa nchini

Aidha amesema mikakati yake ni kuimarisha michezo ikiwemo kujenga uwanja mpya wa kisasa katika eneo la Alabama lilopo ndani ya Jimbo hilo ili kuifanya ligi hiyo kufanyika katika uwanja maalum kila mwaka

Mshindi wa kwanza ambae ni Timu ya Miembeni imebaba kombe na kitita cha Shilingi Milioni mbili huku mshindi wa pili timu ya Kikwajuni ikijinyakulia shilingi Milioni Moja

Nahodha wa Timu ya Mimbeni Seif Salum Said amesema siri ya mafanikio na ushindi huo ni maandalizi mazuri waliyoyafanya pamoja na kufata muongozo kutoka kwa walimu.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.