Na Sheha She.Maelezo. 10.04.2024.
Zaidi ya Wanawake Wajasiriamali 100 wa Mkoa wa Mjini magharibi wamekabidhiwa Majiko ya Gesi ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwa wote.
Akizungumza katika Shughuli ya kukabidhi majiko kwa Wajasiriamali hao huko Rahaleo, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Sharif Ali Sharif amesema majiko hayo yatawawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Waziri Sharif amesema Nishati ya gesi ni muhimu kwa ajili ya kulinda afya za watumiaji pamoja na utunzaji wa Mazingira kutokana na kupunguza matumizi ya rasilimali ya Misitu.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum amewataka Wajasiriamali kulipa kodi kihalali ili kuwewezesha Serikali kupata mapato na kutoa huduma bora kwa Wananchi.
Naye Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita ameishukuru Kampuni ya ORYX ENERGIES kwa mchango wao wa Majiko hayo ambayo yatawarahisishia Wajasiriamali hao katika Shughuli zao na kuwakinga na madhara yatokanayo na matumizi ya kuni ikiwemo moshi.
Naye Meneja Mkuu wa ORYX ENERGIES Kanda ya Zanzibar, Ndg. Shuweikha Khamis Juma amesema Kampuni hiyo imetoa msada huo ili kuwasaidia wanawake hao kuondokana na athari zianazoweza kutokana na matumizi ya nishati ya kuni ikiwemo magonjwa mbalimbali.
Nao Wanawake Wajasiriamali walionufaika na Majiko hayo Wameushukuru Uongozi wa ORYX ENERGIES kwa kuwapatia majiko hayo na kuahidi kuyatumia Vyema ili lengo lililokusudiwa liweze kutimia.
No comments:
Post a Comment