Habari za Punde

ZASP WAHIMIZWA KUTUMIA MTAALA MPYA WA ELIMU

Mkurugenzi Idara ya elimu ya Maandalizi na Msingi Fatma Mode Ramadhani akizungumza na wanachama wa Jumuiya ya  Skuli binafsi wakati wa uchaguzi mkuu wa Jumuiya hiyo  uliofanyika  Skuli Glorious Academy Mpendae.
Baadhi ya wanachama wa Jumuiya ya Skuli binafsi ZASP wakipiga kura kuchagua viongozi wa Jumuiya hiyo huko Skuli ya Glorious Academy Mpendae Wilaya ya Magharibi B.
PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR

Na Fauzia Mussa, Maelezo

Mkurugenzi Idara ya elimu ya maandalizi na msingi Fatma Mode Ramadhani amewataka wamiliki wa Skuli binafsi  kutumia mtaala mpya uliotolewa na wizara ya elimu ili hakikisha watoto wote Zanzibar wanafundishwa kupitia mtaala mmoja.

Akizungumza na wanachama wa jumuiya ya skuli binafsi Zanzibar (ZASP) katika  uchaguzi mkuu wa mwaka wa jumuiya hiyo  uliofanyika Skuli ya Glorious Mpendae Wilaya ya Magharibi B  amesema kufanya hivyo kutawasaidia wanafunzi hao kujifunza mambo mbalimbali  ya Nchi yao ambayo yamo katika mtaala huo.

" Mtaala huu utawasaidia watoto kuweza kujua historia ya Nchi yao pamoja na kuujua utamaduni silka na lugha ya yao"Ameeleza

Sambamba na hayo aliwataka wanachama wa jumuiya hiyo kuchagua viongozi bora na imara watakaowawakikisha vyema katika kusimamia malengo ya jumuiya hiyo.

Akizungumzia maadili katika mahafali ya skuli hizo  Mkurugenzi huyo aliwataka wamiliki wa skuli binafsi kupunguza muda wa hafla hizo na kupunguza kuwashirikisha wanafunzi katika Sanaa na burudani hasa za kisasa badala yake kuitumia siku hiyo kuonesha taaluma waliyoipata wanafunzi hao katika skuli hizo .

"Siku za mahafali  wazazi wanahitaji na kutamani kuona  nini  watoto wao wamepata kuhusiana na elimu ndani ya mwaka mzima wakiwa skulini hapo."

Mwenyekiti wa Jumuiya ya ZASP Kaithar Muhammed said amesema  lengo kuu la kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ni kuimarisha na kuboresha kiwango cha elimu kwa wanafunzi wa skuli binafsi za zanzibar ikiwa ni hatua ya kuuunga mkono juhudi za Wizara ya elimu kwa kupitia ushirikiano kati ya Skuli binafsi na taasisi nyengine za kitaifa na kimataifa.

"Jumuiya hiii ni kwa ajili ya  kukuza mashirikiano kati ya skuli zetu na kuwa kiungo madhubuti cha mawasiliano kati ya  wananchama na  Wizara ya elimu na itaisaidia kuzisimamia skuli binafsi kuhakikisha wanafata mtaala wa wizara ya elimu,".   Alifafanua

Aidha Mwenyekiti huyo kwaniaba ya viongozi  wenziwe waliochaguliwa wameahidi kufanya kazi kwa uaminifu na mashirikiano na wanachama ili kufikia malengo ya kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo.

Wanachama wa Jumuiya hiyo wamesema  ili Jumuiya iweze kudumu uwazi, uwajibikaji na mashirikiano kati ya viongozi wa Jumuiya na wanachama unahitajika.

Aidha wamewaomba viongozi waliochaguliwa kuongoza jumuiya hiyo kuzichukua changamoto za wanachama na kuzifanyia kazi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa

Hata hivyo wamezishauri skuli binafsi ambazo hazijajiunga na jumuiya hiyo kujiunga ili kuwa rahisi kufikiwa na fursa mbalimbali kwani jumuiya hiyo ni daraja kati yao na Serikali kupitia Wizara ya elimu.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.