Habari za Punde

Rais Samia Suluhu Hassan asaini Kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran hapa nchini mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Ubalozi huo Oysterbay Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran nchini Tanzania kufuatia Kifo cha Rais wa Nchi hiyo Hayati Ebrahim Raisi kilichotokana na ajali ya Helikopta nchini Iran. Rais Samia alisaini Kitabu hicho katika Ubalozi wa Iran uliopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2024. Kushoto ni Balozi wa Iran hapa nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran hapa nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Nchi hiyo uliopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran hapa nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Nchi hiyo uliopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran hapa nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh pamoja na Maafisa Mbalimbali wa Ubalozi huo mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Nchi hiyo uliopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2024.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.