Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hissein Mwinyi Azindua Bohari Kuu ya Kwanza Kupokera na Kuhifadhi Gesi Zanzibar ya Kampuni ya Oryx Gas Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja

MUONEKANO wa Bohari ya Kwanza Zanzibar ya Kupokea na Kuhifadhi Gesi Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja iliyofunguliwa leo 27-6-2024 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Bohari Kuu ya Kupokea Gesi Mangapwani ya Kampuni ya Oryx Gas Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya uzinduzi wa Bohari hiyo uliofanyika leo 27-6-2024, na (kushoto kwa Rais) Mkurugenzi Mkuu wa VIGOR Mhe. Toufiq Salim Turky na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Rashid Hadid Rashid
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Vigor Mhe. Toufiq Salim Turky (kushoto) kuzindua Bohari ya kwanza ya Kupokea na Kuhifadhi Gesi ya Kampuni ya Oryx Gas Zanzibar, uzinduzi huo uliyofanyika leo 27-6-2024, katika eneo la Bohari hiyo Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuzindua Bohari ya Kwanza ya Kupokea na Kuhifadhia Gesi ya Kampuni ya Oryx Gas Zanzibar Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 27-6-2024 na (kushoto kwa Rais) Mkurugenzi Mkuu wa Vigor Mhe.Toufiq Salim Turky na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Gas Benoit Araman na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwa Rais) Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar Mhe. Shaib H.Kaduara na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Rashid Hadid Rashid na Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndg. Khamis Mbeto.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea eneo la Bohari Kuu la Kupokea na Kuhifadhi Gesi Mangapwani la Kampuni ya Oryx Gas Zanzibar,baada ya kulizindua leo 27-6-2024,akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Gas. Bw.Benoit Araman
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Project Meneja wa Kampuni ya Oryx Gas Zanzibar Mhandisi Joseph Soko akitowa maelezo ya picha za eneo la Bohari Kuu a Kupokea na Kuhifadhi Gesi Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati wa uzinduzi huo uliyofanyika leo 27-6-2024 Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja

WAGENI waalikwa wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kulizindua Bohari Kuu la Kwanza la Kupokea na Kuhifadhi Gesi la Kampuni ya Oryx Gas Zanzibar Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja, uzinduzi huo uliyofanyika leo 27-6-2024
BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kulizindua Bohari Kuu la Kwanza la Kupokea na Kuhifadhi Gesi la Kampuni ya Oryx Gas Zanzibar Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja, uzinduzi huo uliyofanyika leo 27-6-2024
WANANCHI wa Kijiji cha Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kulifungua Bohari la kupokea na Kuhifadhia Gesi Mangapwani, uzinduzi huo uliyofanyika leo 27-6-2024


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.