Habari za Punde

Serikali kwa muda mrefu imekuwa ikichukua juhudi katika kuhakikisha jamii inaishi katika hali ya usalama

Na.Suleym Muhiddin.

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Mgeni Jailani Jecha amesema Serikali kwa muda mrefu imekuwa ikichukua juhudi katika  kuhakikisha jamii inaishi katika hali ya usalama  na kuepukana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.

Akifungua kikao cha kupitia  rasimu ya muongozo wa waendesha Mashtaka wa kesi za udhalilishaji huko katika ukumbi wa BIMA  Mpirani amesema rasimu ya muongozo huo itakapokamilika itasaidia kuleta ufanisi katika uendeshaji wa kesi za udhalilishaji hasa kwa wanawake na watoto.

Amesema ingawa takwimu zinaonesha kuwa kesi za udhalilishaji zimeanza kupungua kwa kiasi kikubwa katika mahkama nchini hata hivyo muongozo utasaidi kesi zinazofikishwa mahakamani kuendeshwa kwa muda mfupi

 Aidha  amewataka waendesha Mashtaka, Polisi na Mahakimu kuhakikisha kuwa wanachunga haki za watu na wala hawapaswi kumuonea kwa kisingizio cha kutaka kumalizika kwa kesi za udhalilishaji na bada yake wafanyekazi zao kwa uadilifu kama sheria  inavyoelekeza pamoja na kufuata misingi ya haki na sharia.

Wakichangia mada ya rasimu hiyo ya muongozo wa waendesha Mashtaka huo… amesema ipo haja katika kuingizwa kipengele cha kumbana malalamikaji aliyefungua kesi na baadae kukataa kuja kutoa ushahidi wake mahakamani kutokana na kumaliza kesi hizo nje ya mahakama kwa kufanya hivyo kunasababisha usumbufu.

Nae mratibu wa kikao .. Bi Rashida Hemed amewataka washiriki wa kikao hicho kuwa huru katika kuchangia mjadala huo ili kupata michango itakayoweza kutengeneza rasimu nzuri itakayotumiwa na waendesha mashtaka wa kesi za udhalilishaji katika utekelezaji wa kazi zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.