Habari za Punde

Siti Abass Ahamasisha Kuazishwa Majukwaa ya Wanawake Kusini Unguja

Na Takdir Ali. Maelezo. 

Mkurugenzi idara ya maendeleo ya jamii, jinsia na watoto, Siti Abasi Ali amewataka Watoto kuchukuwa tahadhari ya kujikinga na vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia katika maeneo yao.

 

Ameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wa mafunzo maalum ya kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya kikatili na udhalilishaji katika Wilaya ya Kusini.

 

Amesema watoto wengi hawana elimu ya kutosha ya kujikinga na matukio hayo jambo ambalo linapelekea kuongezeka kwa vitendo hivyo.

 

Ambapo amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaelimisha watoto hao ili waweze kujitambua na na kufahamu mbinu bora za kujikinga na janga hilo.

 

Mbali na hayo Mkurugenzi Siti amewaagiza Wazazi na Walezi kushirikiana na Waratibu wa Wanawake na Watoto katika Shehia, kutoa elimu ili Watoto waweze kujilinda na ukatili uanaoweza kujitokeza.

 

Nao baadhi ya Watoto waliopatiwa elimu hiyo, wamesema mafunzo hayo ni mazuri na yamekuja yamekuja wakati muafaka na kuahidi kuyafanyia kazi ili malengo yaliokusudiwa na Idara ya maendeleo ya jamii, jinsia na Watoto yaweze kufikiwa.

 

Hata hivyo wameiomba Idara hiyo kuweka utaratibu wa kukutana na Watoto, Wazazi, Wadau na watetezi wa masuala ya Wanawake na Watoto ili waweze kujadili na kupata mbinu bora za kupambana na tatizo hilo.

 

Mafunzo hayo maalum ya kwajengea uwezo wa kujilinda watoto dhidi ya vitendo vya kikatili na udhalilishaji, yameandaliwa na Idara ya Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto na kuwashirikisha Mabaraza ya Watoto wa Shehia ya mbalimbali za Wilaya ya Kusini, ikiwemo Shehia ya Muungoni, Kizimkazi Mkunguni, Muyuni A, B, na C.


Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto Siti Abasi Ali akitoa elimu ya kujikinga na ukatili na udhalilishaji wa Watoto kwa Mabaraza ya Watoto ya Wilaya ya Kusini huko Muungoni Wilaya ya Kusini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.