Habari za Punde

Wanafunzi wa Saikolojia Vyuo Vikuu Zanzibar Wafanya Kongamano

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis  Hafidh akimkabidhi cheti cha shukrani  Mwenyekiti wa Taasisi ya  Inshirah Charitable Organization Zanzibar Kevser Kocadag katika Mkutano Mkuu na Kongamano la wanafunzi wa kada  ya Saikolojia  katika Vyuo vikuu vya Zanzibar lillilofanyika ukumbi wa Studio Rahaleo Mjini Unguja.

Na Fauzia Mussa , Maelezo Zanzibar.

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh amesema kuwepo kwa wanasaikoljia nchini kutasaidia jamii kuondokana na  msongo wa mawazo na kuugua afya ya akili.

 

Akizungumza katika  kongamano la wanafunzi wa  Saikolojia wa  vyuo vikuu Zanzibar Naibu Hafidh amewataka  wataalamu hao kutumia elimu zao kuelimisha   jamii  juu ya athari zinazotokana  na msongo wa  mawazo ili kuweza kujilinda.

 
“Binadamu tunakabiliwa na matatizo mbali mbali kama maradhi na migogoro mambo yanayopelekea msongo wa mawazo hivyo kuwepo kwa wanasaikolojia katika maeneo yetu  kutasaidia  kupunguza  matatizo haya.” Alieleza Naibu Hassan

 

Aidha ameeleza kuwa  wanasaikolojia bado ni watu muhimu  katika maeneo mbalimbali kwani hata wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi sugu, wanahitaji matibabu ya Saikolojia kuweza  kukubaliana na hali hiyo.


Sambamba na hayo amewataka  wanafunzi wa kada hiyo kutumia ujuzi wao kuelimisha  jamii juu ya  athari  za matumizi ya dawa za  kulevya ili kupata taifa lenye  watu  imara.

 

Amefahamisha kuwa vijana wengi wanaotoka katika vituo vya kurekebishia tabia wanarudia kutumia dawa za kulevya kutokana na kukosa matibabu ya saikolojia hivyo kada hiyo ni muhimu na inapaswa kupewa kipaombele.

 

“katika vituo vya kurekebisha tabia (Soba house) hakuna wanasaikolojia kuweza kuwatibu hawa wathirika wa dawa za kulevya hili linachangia wao kurudia tena katika matumizi ya dawa hizo”alisema naibu Waziri


Akitoa nasaha kwa wanafunzi hao  balozi wa Vijana bw. Mohamed  Kassim na Mkuu  wa idara ya  afya ya   saikolojia kutoka chuo kikuu cha Zanzibar (ZU) dkt. khalfan  Mohamed, wamesema kuna  umuhimu mkubwa  wa taasisi za   Serikali na binafsi kuwepo wanasaikolojia ili kuwa salama  katika sehemu  za kazi.

Akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wa kada hiyo  Ramadhan Mohamed Hassan  amesema licha ya kozi hiyo  kuwa  na umuhimu mkubwa kwa jamii lakini  imekua ikakabiliwa na matatizo  mengi  ikiwemo kutokupewa kipaombele katika nafasi  za ajira.

Katika Mkutano  huo mada mbali mbali zilijadiliwa ikiwemo saikolojia ya afya ya  akili, ugonjwa wa msongo baada ya janga na athari za saikolojia za  vitendo  vya udhalilishaji kisaikolojia na ukatili wa kijinsia.

                                          
Balozi wa Vijana Mohammed Kassim akimkabidhi zawadi maalum  Mwenyekiti wa Taasisi ya  Inshirah Charitable Organization Zanzibar katika Mkutano Mkuu na Kongamano la wanafunzi wa kada  ya Saikolojia  katika Vyuo vikuu vya Zanzibar lillilofanyika ukumbi wa Studio Rahaleo Mjini Unguja.
                                         
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis  Hafidh akizungumza na wanafunzi wa Saikolojia katika Mkutano Mkuu na Kongamano la wanafunzi wa kada hiyo katika vyuo vikuu vya Zanzibar lillilofanyika ukumbi wa Studio Rahaleo Mjini Unguja.
 Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis  Hafidh akizungumza na wanafunzi wa Saikolojia katika Mkutano Mkuu na Kongamano la wanafunzi wa kada hiyo katika vyuo vikuu vya Zanzibar lillilofanyika ukumbi wa Studio Rahaleo Mjini Unguja. 

Baadhi ya washiriki wakifuatilia Mkutano mkuu na Kongamano la wanafunzi wa kada ya Saikolojia  katika vyuo vikuu vya Zanzibar lillilofanyika ukumbi wa Studio Rahaleo Mjini Unguja.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia Mkutano mkuu na Kongamano la wanafunzi wa kada ya Saikolojia  katika vyuo vikuu vya Zanzibar lillilofanyika ukumbi wa Studio Rahaleo Mjini Unguja.

PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.