Habari za Punde

WAZIRI WA BIASHARA AZINDUA MFUMO WA UASILISHAJI MASHAURI YA RUFAA ZA USHINDANI.ndani

Na Takdir Ali. Maelezo. 05.06.2024.

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaabani amewataka wafanyabiashara kupeleka mashauri yao kwa Baraza la Ushindani Halili wa Biashara Zanzibar (ZFCT) ikiwa hawakuridhika na maamuzi yaliotolewa na watoa huduma ili kuweza kupata haki zao.

 

Ameyasema wakati alipokuwa akizinduzi Mfumo wa Uasilishaji mashauri ya Rufaa za Ushindani huko huko katika ukumbi wa sheikh Idris Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini.

 

Amesema baadhi ya wakati watoa huduma ikiwemo ZURA, ZFDA na ZMA wanatoa huduma ambazo zinawakwaza Wafanyabiashara hivyo ni vyema kulitumia Baraza hilo kupeleka rufaa zao ili waweze kupata haki zao.

 

Aidha Mhe. Shaaban ameliomba Baraza la ushindani halali wa biashara Zanzibar (ZFCT) kutoa elimu kwa Wananchi ili waweze kulitumia Baraza hilo na kupeleke malalamiko yao ili yaweze kufanyiwa kazi na kupata haki zao.

 

Hata hivyo ameziagiza Taasisi na Mamlaka zilizo chini ya Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda kuanzisha mifumo ili kutoa huduma kwa urahisi na kuondosha malalamiko, Rushwa na Udanganyifu.

 

Mbali na hayo amesema lengo la kuanziswa ZFCT ni kujenga mazingira mazuri ya biashara ili kuondosha Malalamiko na nchi kuweza kupiga hatua za maendeleo.

 

Mapema akitoa maelezo Mrajisi wa Baraza la Ushindani halali Zanzibar (ZFCT) Fatma Gharib Haji amesema Mfumo huo unatarajia kuondosha changamoto na malalamiko katika ufanyaji wa kazi na kuweza kurahisisha upatikanaji wa huduma, salama na haraka.

 

Aidha amesema lengo la Baraza hilo ni kumlinda mteja asipate bidhaa isiokuwa na kiwango na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa urahisi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.