Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Akiendelea na Ziara Yake Pemba Kutembelea Miradi ya Maendeleo

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na wananchi wa Kiuyu Mbuyuni Wilaya wa Micheweni Pemba mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Barabara ya Micheweni- Kiuyu Maziwango'mbe inayojengwa na Mkandarasi Kampuni ya IRIS Contraction Company ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kukagua miradi ya maendeleo inayojengwa Kisiwani Pemba.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya Comfix & Engineering anaejenga Bandari ya Shumba Mjini kuhakikisha wanamaliza ujenzi kwa wakati uliopangwa na kwa kiwango kilichokusundiwa na kushindwa kufanya hivyo atakuwa amejinyima fursa ya kuendelea kufanya kazi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akikagua maendeleo ya ujenzi wa bandari hiyo Mhe. Hemed amesema eneo la Bandari ya Shumba lina uhitaji mkubwa kwa wananchi wanaoishi hapo hasa ukizingatia shuhuli zao nyingi za kiuchumi zinategemea Bandari kwa kutoa na kupokea bidhaa mbali  mbali kutoka nchi jirani.

Mhe.Hemed amefahamisha kuwa kukamilika kwa bandari hio itatoa fursa ya kupatikana kwa  ajira kwa vijana wazawa na wa vijiji jirani sambamba na  kuwaondolea changamoto ya kusafiri masafa ya mbali kwa ajili ya kusafirisha na kupokea mizo yao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema endapo Kampuni ya Comfix itashindwa kukamilisha mradi kwa wakati uliopangwa italazimika kuilipa Serikali kutokana na hasara watakayoisababishia kwa kipindi chote ambacho  wamefanya kazi nje ya makubaliano ya kimkataba.

Wakati huo huo Makamo ya wa Pili wa Rais amekagua ujenzi wa barabara ya Micheweni - Kiuyu Maziwango'mbe yenye urefu wa Km 7.5 inayojengwa na Mkandarasi Kampuni ya Iris Contraction Company inayotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi wa September.

Mhe.Hemed ameseme Serikali ya Awamu ya Nane (8) inayoongozwa na Rais Dkt Hussen Mwinyi imejipanga kuzijenga kwa kiwango cha lami barabara zote zilizomo latika mpango mkakati mjini na vijijini ili kuharakisha upatikanaji wa maendelo kwa wananchi wote  wa zanzibar.

Sambamba na Hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amemtaka Mkandarasi Salim Construction Ltd anaejenga mradi wa Skuli za Sekondari Konde na Kifundi kuongeza kasi katika ujenzi wa mradi hio pamoja na  kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha wanakabidhi miradi hio kwa wakati uliopangwa.

Amesema dhamira ya Rais Dkt Mwinyi ni kuona wanafunzi wanasoma katika mazuri yenye miundombinu bora inayokidhi mahitaji yote ya kufundishia na kujisomea ili Zanzibar iwe na wasomi bora wa fani mbali mbali.

Aidha Makamo wa Pili wa Rais amewataka wananchi wa Jimbo la Konde kuacha kusikiliza maneno yasiyo nantija kwao na badala yake wamuunge mkono Dkt Mwinyi katika kuhakikisha Taifa linasonga mbele kimaendeleo.

Kwa upande wao mawaziri wenye dhamana ya kusimamia miradi hio wamesema dhamira ya serikali ni kuhakikisha inawaletea maendelelo wananchi wake hivyo wakiwa ni wenye dhamana ya wizara hizo watahakikisha wanasimamia vyema miradi hio ili iweze kukamilika kwa wakati uliopangwa na ubora uliokusudiwa kwa lengo la kuwaondolea changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi wote wa Zanzibar.

Wamesema Rais Dkt Mwinyi ametekeleza kwa vitendo yale yote aliyoyaaahidi kwa wananchi na ilivyoelekezwa katika ilani ya chama cha Mapinduzi hivyo ni wajibu wa wananchi kuendelea kumuunga mkono ili aendelee kuiletea Zanzibar Maendeleo.

Kwa upande wao wakandarasi wanaojenga miradi mbali mbali ikiwemo wa Bandari ya Shumba na barabara ya Micheweni- Kiuyu Maziwango'mbe na Skuli za sekondari Konde na Kifundi wamemuahidi Mhe. Makamu wa Pili wa Rais kuwa watafanya kazi usiku na mchana na kuongeza rasilimali watu na vifaa ili kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati ujenzi wa miradi hiyo.

Wamesema licha ya changamoto ya uhaba wa maeneo ya kufanyia kazi na changamoto ya mvua zilizokwamisha ujenzi wa  miradi hio wameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwaamini kuwa wataijenga miradii hiyo kwa viwango na ubora wa  hali ya juu ili iweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu kwa faida ya vizazi vya sasa na baadae.

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar amekamilisha ziara yake katika Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa kukagua miradi mbali mbali ikiwemo MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA MICHEWENI- KIUYU MAZIWANGO'MBE, BARABARA YA MICHEWENI- SHUMBA MJINI, BANDARI YA SHUMBA MJINI, SOKO LA WAJASIRIAMALI TUMBE, BARABARA YA MAPOFU- TUMBE, SKULI YA SEKONDARI KONDE NA SKULI YA SEKONDARI KIFUNDI.

 

Imetolewa na kitengo cha Habari (OMPR)

LEO tarehe 30.07.2024

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.