Waziri wa Maji Nishati na Madini Shaib Hassan Kaduwara akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Uzinduzi wa Ripoti ya Jiolojia na Utafiti wa Madini uliofanyika Zanzibar,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Zura Maisara Zanzibar.
Baaadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Waziri wa Maji Nishati na Madini Shaib Hassan Kaduwara na Waandishi wa Habari kuhusiana na Taarifa ya Uzinduzi wa Ripoti ya Jiolojia na Utafiti wa Madini uliofanyika Zanzibar,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Zura Maisara Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.10/09/2024.
Na Sabiha Khamis Maelezo 10.09.2024
Wizara ya Maji, Nishati na Madini ,Zanzibar kwa kushirikiana na Wizara ya Madini Tanzania Bara kupitia Taasisi ya Jiolajia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ilifanya utafiti wa awali wa Jiolojia katika Visiwa vya Unguja na Pemba.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Shaib Hassan Kaduara amesema zoezi hilo ni moja ya matunda ya makubaliano ya Mashirikiano (MoU) baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara zake kwa kuibua fursa mbali mbali.
Amesema Utafiti huo ulilenga kuandaa Ramania ya Jiolojia ya Visiwa vya Unguja na Pemba ambao haukuepo hapo awali na dunia kwa sasa inatilia mkazo madini ya kimkakati na Viwanda
Aidha, amesema miongoni mwa mafanikio makubwa ya utafiti huo kubaini maeneo yenye viashiria mbali mbali vya madini katika visiwa vya Zanzibar ambavyo vitaiwezesha Wizara kuendelea na tafiti za kina ili kuwa na taarifa za kutosha kuhusu kiwango cha madini kilichopo.
"Kutokana na Jiografia na Jiolojia ya Zanzibar, ramani ya Jiolojia iliyochorwa imeweza kuibua vivutio vya utalii wa jiolojia na kuvitolea maelezo ya kina visiwa vikubwa na vidogo" alisema Waziri Kaduara.
Amefafanua kuwa utafiti huo umeweza kutambua miamba inayoweza kuwa chanzo cha maji ambapo baadhi ya miamba hiyo ina sifa ya kupitisha maji na kuhifadhi maji chini ya ardhi.
Amebainisha kuwa maeneo ya Visiwa vya Zanzibar, inaweza kukumbwa na majanga ya asili ya jiolojia ya kudidimia kwa ardhi kutokana na hali ya miamba inayolika kirahisi na maji ya mvua pamoja na mafuriko ya fukwe yatokanayo na athari za sunami na kimbunga.
Uzinduzi wa Ripoti ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Zanzibar unatarajiwa kufanyika tarehe 12 Septemba 2024 katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport Zanzibar Mgeni rasmin anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
No comments:
Post a Comment