Chama cha Majaji na Mahakama Zanzibar (ZAJOA) kimewataka wanasiasa kuacha kutumia majukwaa ya kisiasa kwa kutoa matamshi yanayoashiria kuharibu twasira ya Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Hayo yameelezwa na Rais wa Chama hicho Jaji Salma Ali Hassan wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kufuatia matamshi yanayotolewa na baadhi ya Viongozi wakuu wa Vyama vya siasa.
Amesema Mahakama Kuu ni chombo huru kiilichopewa mamlaka ya utoaji haki kama kinavoenesha kifungu 5A cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Aidha amesema kwamba iyeleweke kuwa Mahakama Kuu ya Zanzibar haijinasibishi wala kufuata upande wowote wa kisiasa na wala haifanyi majukumu yake ya utoaji haki kwa kupokea maagizo kutoka kwa viongozi wakuu wa Serikali au kwa mtu mwengine yeyote.
Ameongeza kuwa kupitia matamshi hayo na tuhuma ambazo zimekuwa zinanasibishwa na utendaji kazi wa Mahakama ya Zanzibar,Chama cha Majaji na Mahakama kimekua kikitafakari tuhuma na matamshi hayo ya wanasiasa na kuamini kuwa kadri uhuru wa kujieleza utakapozoeleka mori na munkari kwa wanasiasa na watumiaji wa majukaa hayo utapungua na busara za viongozi zitafikia mwisho (zitatamalaki)
Katika hatua nyengine Rais wa Chama hicho amesema kuwa chama kinaheshimu uhuru wa kutoa maoni kama ilivyoelezwa kifungu cha 18 cha Katiba ya Zanzibar ,ya 1984 lakini uhuru huo usitumike vibaya wala usivuke mipaka na kuharibu,kuchochea ama kupotosha taswira na uhuru wa Mahakama katika utekelezaji wa majukumu ya utoaji wa haki.
Hata hivyo Chama hicho kinasisitiza kuwa ni vyema kila mmoja akatumia uhuru wake wa kutoa maoni kwa kuzingatia kuwa hauvuki mipaka na kuvunja ama kubomoa au kwa makusudi au kwa kudhamiria taswira ya chombo au mtu mwengine.
No comments:
Post a Comment